-
Wokovu Unawezekana Mungu Alipizapo KisasiMnara wa Mlinzi—1989 | Mei 15
-
-
Ni waadilifu na waaminifu tu watakaoendelea kuishi. Yehova anahakikishia Habakuki jambo hili. Ingawa huenda ikaonekana kuna ukawivu, kwenye wakati wa Mungu uliowekwa njozi ya kiunabii “haina budi kuja.” Adui mwenye kimbelembele anayeteka nyara za mataifa hatafikia mradi wake. Kweli kweli, Wakaldayo hawataendelea bila kuadhibiwa.—2:2-5.
-
-
Wokovu Unawezekana Mungu Alipizapo KisasiMnara wa Mlinzi—1989 | Mei 15
-
-
○ 2:5—Wababuloni waliunganika kuwa mtu mmoja wa ujumla ambaye alitumia jeshi lake la kivita kuyashinda mataifa. Yeye alitamani ushindi zaidi na zaidi wa kijeshi, kama vile Sheoli na kifo huwa tayari sikuzote kupokea majeruhi wengi zaidi. (Linganisha Mithali 30:15, 16.) Yeye alilewa ulevi wa kutaka sana ushindi, kana kwamba aliongozwa na unywaji wa kupindukia. Lakini vita vyake vya ushindi vilimalizika wakati Babuloni ilipoanguka katika 539 K.W.K.
-