Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Siku ya Hukumu ya Yehova I Karibu!
    Mnara wa Mlinzi—2001 | Februari 15
    • 6-8. Ni nini kilichotabiriwa kwenye Sefania 1:4-6, na unabii huo ulitimizwaje katika Yuda ya kale?

      6 Likitabiri matendo ya Mungu dhidi ya waabudu wasio wa kweli, andiko la Sefania 1:4-6 lasema hivi: “Nitaunyosha mkono wangu juu ya Yuda, na juu ya watu wote wakaao Yerusalemu; nami nitayakatilia mbali mabaki ya Baali, yasionekane mahali hapa, na hilo jina la Wakemari pamoja na makuhani; na wale walisujudiao jeshi la mbinguni juu ya dari za nyumba; na hao waabuduo, waapao kwa BWANA na kuapa pia kwa Malkamu; na hao waliorudi nyuma, na kuacha kumfuata BWANA; na hao wasiomtafuta BWANA, wala kumwulizia.”

  • Siku ya Hukumu ya Yehova I Karibu!
    Mnara wa Mlinzi—2001 | Februari 15
    • 9. (a) Jumuiya ya Wakristo ina hatia gani? (b) Tofauti na watu wa Yuda wasio waaminifu, twapaswa kuazimia kufanya nini?

      9 Huenda yote hayo yakatukumbusha Jumuiya ya Wakristo, ambayo imekolea ibada isiyo ya kweli na unajimu. Nako kule kudhabihu mamilioni ya watu kwenye madhabahu ya vita vinavyoungwa mkono na makasisi ni jambo lenye kuchukiza kwelikweli! Na tusiwe kamwe kama watu wasio waaminifu wa Yuda, ‘walioacha kumfuata Yehova,’ wakawa wasiojali chochote na kuacha kabisa kumtafuta au kutafuta mwelekezo wake. Badala yake, na tudumishe uaminifu-maadili wetu kwa Mungu.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki