Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Siku ya Hukumu ya Yehova I Karibu!
    Mnara wa Mlinzi—2001 | Februari 15
    • 14. Mungu angewachunguza kwa undani kadiri gani wale wanaodai kuwa waabudu wake?

      14 Yehova angewachunguza kwa undani kadiri gani wale wanaodai kuwa wanamwabudu? Unabii huo waendelea kusema hivi: “Kisha itakuwa wakati ule, nitauchunguza Yerusalemu kwa taa; nami nitawaadhibu watu walioganda juu ya sira zao; wasemao katika mioyo yao, BWANA hatatenda mema, wala hatatenda mabaya. Na huko utajiri wao utakuwa mateka, na nyumba zao zitakuwa ukiwa; naam, watajenga nyumba, lakini hawatakaa ndani yake; nao watapanda mizabibu, lakini hawatakunywa divai yake.”—Sefania 1:12, 13.

  • Siku ya Hukumu ya Yehova I Karibu!
    Mnara wa Mlinzi—2001 | Februari 15
    • 16. Ni nini ambacho kingetukia wakati ambapo hukumu ya Mungu ingetekelezwa dhidi ya Yuda, na kujua hivyo kwapasa kutuathirije?

      16 Waasi-imani wa Yuda walionywa kwamba Wababiloni wangepora mali zao, wangefanya nyumba zao ukiwa, na kutwaa matunda ya mashamba yao ya mizabibu. Mali za kimwili hazingekuwa na thamani yoyote wakati ambapo hukumu ya Mungu ingetekelezwa dhidi ya Yuda. Ndivyo itakavyokuwa siku ya hukumu ya Yehova itakapoujia mfumo huu wa mambo. Kwa hiyo, na tuwe na mtazamo wa kiroho na ‘kuweka hazina mbinguni’ kwa kuendelea kutanguliza utumishi wa Yehova maishani mwetu!—Mathayo 6:19-21, 33.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki