-
“Fulizeni Kunitarajia”Mnara wa Mlinzi—1996 | Machi 1
-
-
13. Sefania alitangaza ujumbe gani wenye hukumu dhidi ya Moabu, Amoni, na Ashuru?
13 Kupitia nabii wake Sefania, Yehova alionyesha hasira yake pia dhidi ya mataifa yaliyokuwa yamewatendea watu wake vibaya. Alitangaza hivi: “Mimi nimeyasikia matukano ya Moabu, na dhihaka za wana wa Amoni, ambazo kwa hizo wamewatukana watu wangu, na kujitukuza juu ya mpaka wao. Basi kama niishivyo, asema BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, Hakika Moabu atakuwa kama Sodoma, na wana wa Amoni kama Gomora, yaani, milki ya upupu, na mashimo ya chumvi, ukiwa wa daima. . . . Naye atanyosha mkono wake juu ya upande wa kaskazini, na kuiangamiza Ashuru; naye ataufanya Ninawi kuwa ukiwa, kuwa mahali pakavu kama jangwa.”—Sefania 2:8, 9, 13.
14. Kuna uthibitisho gani kwamba mataifa ya kigeni ‘yalijitukuza’ juu ya Waisraeli na Mungu wao, Yehova?
14 Moabu na Amoni walikuwa maadui wa Israeli wa tangu zamani. (Linganisha Waamuzi 3:12-14.) Jiwe la Moabu, lililo katika Louvre Museum katika Paris, lina maandiko yenye taarifa ya kujisifu iliyotolewa na Mfalme Mesha wa Moabu. Yeye asimulia kwa majivuno jinsi alivyotwaa majiji kadhaa ya Israeli kwa msaada wa mungu wake Kemoshi. (2 Wafalme 1:1) Yeremia, aliyeishi wakati wa Sefania, alisema juu ya Waamoni kuwa wanakalia eneo la Israeli la Gadi katika jina la mungu wao Malkamu. (Yeremia 49:1) Kuhusu Ashuru, Mfalme Shalmanesa 5 alizingira na kuteka Samaria karibu karne moja kabla ya siku ya Sefania. (2 Wafalme 17:1-6) Baadaye kidogo, Mfalme Senakeribu alishambulia Yuda, akateka majiji mengi yenye ngome, na hata kutisha Yerusalemu. (Isaya 36:1, 2) Msemaji wa mfalme wa Ashuru alijitukuza juu ya Yehova alipokuwa akidai Yerusalemu lisalimu amri.—Isaya 36:4-20.
-
-
“Fulizeni Kunitarajia”Mnara wa Mlinzi—1996 | Machi 1
-
-
15. Yehova angeaibishaje miungu ya mataifa yaliyojitukuza juu ya watu wake?
15 Zaburi 83 hutaja mataifa kadhaa, kutia ndani Moabu, Amoni, na Ashuru, waliojitukuza juu ya Israeli, na kusema hivi kwa kujigamba: “Njoni, tuwakatilie mbali wasiwe taifa, na jina la Israeli halitakumbukwa tena.” (Zaburi 83:4) Nabii Sefania alitangaza kwa moyo mkuu kwamba mataifa hayo yote yenye kiburi na miungu yayo yangeaibishwa na Yehova wa majeshi. “Mambo hayo yatawapata kwa sababu ya kiburi chao, kwa kuwa wamewatukana watu wa BWANA wa majeshi, na kujitukuza juu yao. BWANA atakuwa mwenye kuwatisha sana; kwa maana atawafisha kwa njaa miungu yote ya dunia; na watu watamsujudia yeye, kila mtu toka mahali pake; naam, nchi zote za mataifa.”—Sefania 2:10, 11.
-
-
“Fulizeni Kunitarajia”Mnara wa Mlinzi—1996 | Machi 1
-
-
18. (a) Hukumu ya kimungu ilitekelezwaje juu ya Yerusalemu, na kwa nini? (b) Unabii wa Sefania kuhusu Moabu na Amoni ulitimizwaje?
18 Wayahudi wengi waliofuliza kumtarajia Yehova pia waliishi wakaona hukumu zake zikitekelezwa juu ya Yuda na Yerusalemu. Kuhusu Yerusalemu, Sefania alikuwa ametabiri: “Ole wake yeye aliyeasi na kutiwa unajisi, mji wa udhalimu! Hakuitii sauti; hakukubali kurudiwa; hakumwamini BWANA; hakumkaribia Mungu wake.” (Sefania 3:1, 2) Kwa sababu ya kukosa uaminifu, Yerusalemu lilizingirwa mara mbili na Wababiloni na hatimaye kutekwa na kuharibiwa katika 607 K.W.K. (2 Mambo ya Nyakati 36:5, 6, 11-21) Kwa habari ya Moabu na Amoni, kulingana na Yosefo, mwanahistoria Myahudi, katika mwaka wa tano baada ya Yerusalemu kuanguka, Wababiloni walipiga vita nao na kuwashinda. Wao nao walipotelea mbali, kama ilivyotabiriwa.
-
-
“Mikono Yako Isilegee”Mnara wa Mlinzi—1996 | Machi 1
-
-
3. Ni nini laweza kusemwa juu ya viongozi wengi wa kilimwengu na serikali za kisiasa leo, na Sefania alitoa unabii juu ya nini?
3 Wengi wa viongozi wa kisiasa wa Jumuiya ya Wakristo hupenda kuonwa makanisani. Lakini kama “wakuu,” wa Yuda baadhi yao hutumia watu vibaya kama “simba wangurumao” na “mbwa mwitu” wenye pupa. (Sefania 3:1-3) Watumishi wao wa kisiasa wenye kutaka upendeleo wao ‘wanaijaza nyumba ya Bwana wao udhalimu na udanganyifu.’ (Sefania 1:9) Rushwa na ufisadi umeenea. Kwa habari ya serikali za kisiasa zilizo ndani na nje ya Jumuiya ya Wakristo, idadi yenye kuongezeka ya serikali hizo ‘zinajitukuza’ juu ya watu wa Yehova wa majeshi, Mashahidi wake, zikiwaona kuwa “farakano” lenye kudharauliwa. (Sefania 2:8; Matendo 24:5, 14, NW) Kuhusu viongozi wote wa kisiasa kama hao na wafuasi wao, Sefania alitoa unabii huu: “Fedha yao wala dhahabu yao havitaweza kuwaokoa katika siku ile ya ghadhabu ya BWANA; bali nchi yote pia itateketezwa kwa moto wa wivu wake; maana atawakomesha watu wote wakaao katika nchi hii, naam, ukomo wa kutisha.”—Sefania 1:18.
-