-
“Fulizeni Kunitarajia”Mnara wa Mlinzi—1996 | Machi 1
-
-
“Fulizeni Kunitarajia”
16. (a) Ni kwa akina nani kuja kwa siku ya Yehova kulikuwa chanzo cha shangwe, na kwa nini? (b) Ni amri gani yenye kuamsha iliyotolewa kwa mabaki waaminifu?
16 Huku ulegevu wa kiroho, shaka, ibada ya sanamu, ufisadi, na ufuatiaji wa vitu vya kimwili ukienea miongoni mwa viongozi na wakazi wengi wa Yuda na Yerusalemu, yaonekana kwamba baadhi ya Wayahudi waaminifu walisikiliza unabii mbalimbali wenye onyo aliotoa Sefania. Wao walisikitishwa na matendo ya kuchukiza ya wakuu, waamuzi, na makuhani wa Yuda. Matangazo ya Sefania yalikuwa chanzo cha faraja kwa hawa waaminifu-washikamanifu. Badala ya kuwa kisababishi cha huzuni, kuja kwa siku ya Yehova kulikuwa chanzo cha shangwe kwao, kwa sababu kungekomesha matendo hayo yenye kuchukiza. Hawa mabaki waaminifu walitii amri ya Yehova ya kuwaamsha: “Basi ningojeni [“fulizeni kunitarajia,” NW] asema BWANA, hata siku ile nitakapoondoka kuteka mateka; maana nimeazimia kuwakusanya mataifa, ili nizikutanishe falme, nipate kuwamwagia ghadhabu yangu; naam, ukali wote wa hasira yangu.”—Sefania 3:8.
17. Ni lini na ni jinsi gani jumbe zenye hukumu za Sefania zenye hukumu zilianza kutimizwa dhidi ya mataifa?
17 Wale waliotii onyo hilo hawakushangaa. Wengi waliishi wakaona utimizo wa unabii wa Sefania. Katika 632 K.W.K., Ninawi lilitekwa na kuharibiwa na muungano wa Wababiloni, Wamedi, na vikundi kutoka kaskazini, labda Waskaithia. Mwanahistoria Will Durant asimulia: “Jeshi la Wababiloni chini ya Nabopolasari liliungana na jeshi la Wamedi chini ya Siaksaresi na vikundi vya Waskaithia kutoka Kaukasi, na kwa urahisi na wepesi wenye kushangaza waliteka ngome za kaskazini. . . . Kwa pigo moja Ashuru ilipotea katika historia.” Hivyo ndivyo alivyotabiri Sefania.—Sefania 2:13-15.
18. (a) Hukumu ya kimungu ilitekelezwaje juu ya Yerusalemu, na kwa nini? (b) Unabii wa Sefania kuhusu Moabu na Amoni ulitimizwaje?
18 Wayahudi wengi waliofuliza kumtarajia Yehova pia waliishi wakaona hukumu zake zikitekelezwa juu ya Yuda na Yerusalemu. Kuhusu Yerusalemu, Sefania alikuwa ametabiri: “Ole wake yeye aliyeasi na kutiwa unajisi, mji wa udhalimu! Hakuitii sauti; hakukubali kurudiwa; hakumwamini BWANA; hakumkaribia Mungu wake.” (Sefania 3:1, 2) Kwa sababu ya kukosa uaminifu, Yerusalemu lilizingirwa mara mbili na Wababiloni na hatimaye kutekwa na kuharibiwa katika 607 K.W.K. (2 Mambo ya Nyakati 36:5, 6, 11-21) Kwa habari ya Moabu na Amoni, kulingana na Yosefo, mwanahistoria Myahudi, katika mwaka wa tano baada ya Yerusalemu kuanguka, Wababiloni walipiga vita nao na kuwashinda. Wao nao walipotelea mbali, kama ilivyotabiriwa.
19, 20. (a) Yehova alithawabishaje wale waliofuliza kumtarajia? (b) Kwa nini matukio haya yanatuhusu, na ni mambo yapi yatakayozungumzwa katika makala ifuatayo?
19 Utimizo wa jambo hili na mambo mengine madogo-madogo ya unabii wa Sefania uliimarisha imani ya Wayahudi na wasio-Wayahudi waliofuliza kumtarajia Yehova. Miongoni mwa wale waliookoka uharibifu uliopata Yuda na Yerusalemu walikuwa Yeremia, Ebed-Meleki Mwethiopia, na nyumba ya Yehonadabu, Mrekabu. (Yeremia 35:18, 19; 39:11, 12, 16-18) Wayahudi waaminifu waliokuwa katika uhamisho na wazao wao, walioendelea kumngoja Yehova, walikuja kuwa sehemu ya mabaki wenye furaha waliokombolewa kutoka Babiloni katika 537 K.W.K. na kurudi Yuda kuanzisha tena ibada safi.—Ezra 2:1; Sefania 3:14, 15, 20.
-
-
“Mikono Yako Isilegee”Mnara wa Mlinzi—1996 | Machi 1
-
-
2. Kuna ulinganifu gani kati ya hali zilizokuwa katika siku ya Sefania na hali iliyoko katika Jumuiya ya Wakristo leo?
2 Leo, uamuzi wa kihukumu wa Yehova ni kukusanya mataifa kwa ajili ya uharibifu mkubwa zaidi kuliko ule wa siku ya Sefania. (Sefania 3:8) Mataifa yale yanayodai kuwa ya Kikristo hasa yanastahili adhabu machoni pa Mungu. Kama Yerusalemu lilivyoadhibiwa vikali kwa ajili ya kukosa uaminifu kwa Yehova, ndivyo Jumuiya ya Wakristo ni lazima iadhibiwe na Mungu kwa sababu ya njia zayo zenye kupotoka. Hukumu za kimungu zilizotangazwa dhidi ya Yuda na Yerusalemu katika siku ya Sefania hutumika hata kwa nguvu zaidi dhidi ya makanisa na mafarakano ya Jumuiya ya Wakristo. Wao pia wamechafua ibada safi kwa mafundisho yao yenye kumvunjia Mungu heshima, mengi yakiwa ni ya asili ya kipagani. Wamedhabihu mamilioni ya wana wao wenye afya nzuri katika madhabahu ya kisasa ya vita. Isitoshe, wakazi wa kifanani cha Yerusalemu huchanganya ule uitwao eti Ukristo pamoja na unajimu, mazoea ya uwasiliani-roho na ukosefu wa adili katika ngono zenye kupotoka, matendo yafananayo na ibada ya Baali.—Sefania 1:4, 5.
-