-
Maswali Kutoka kwa WasomajiMnara wa Mlinzi—2014 | Novemba 15
-
-
Kwa kweli, andiko la Ufunuo 11:1 na 2 linahusianisha matukio hayo na wakati ambapo hekalu la kiroho lingepimwa, au kukaguliwa. Andiko la Malaki sura ya 3 linataja ukaguzi kama huo wa hekalu la kiroho, uliofuatwa na kipindi cha kutakasa. (Mal. 3:1-4) Kazi hiyo ya kukagua na kutakasa ilichukua muda gani? Ilianza mwaka wa 1914 mpaka mwanzoni mwa 1919. Kipindi hicho kinatia ndani siku 1,260 (miezi 42) na siku tatu na nusu za mfano zinazotajwa katika Ufunuo sura ya 11.
-