Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kujaribu na Kupepeta Nyakati za Kisasa
    Mnara wa Mlinzi—1987 | Juni 15
    • Kujaribu na Kupepeta Nyakati za Kisasa

      “Ni nani atakayestahimili siku ya kuja kwake? au ni nani atakayesimama atakapoonekana yeye?”​—MALAKI 3:2.

      1. Yehova alipokuja kwenye hekalu la kiroho katika nyakati za kisasa, yeye alipata kuona nini, jambo hilo likitokeza swali gani?

      WAKATI “Bwana [wa kweli]” alipokuja kwenye hekalu la kiroho akiwa pamoja na “mjumbe wa agano” wake muda mfupi baada ya Ufalme kusimamishwa katika mbingu katika 1914, Yehova alipata kuona nini? Watu wake walihitaji kusafishwa na kutakaswa. Je! wao wangejitiisha wenyewe kwa jambo hili na kuvumilia utakasaji wo wote uliohitajiwa wa tengenezo lao, utendaji, mafundisho, na mwenendo? Kama anavyosema Malaki: “Ni nani atakayestahimili siku ya kuja kwake? Au ni nani atakayesimama atakapoonekana yeye?”​—Malaki 3:1, 2.

  • Kujaribu na Kupepeta Nyakati za Kisasa
    Mnara wa Mlinzi—1987 | Juni 15
    • 3. Kufikia kiangazi cha 1918, ni nini iliyokuwa hali ya mashahidi wa Mungu?

      3 Yehova alipoambatana pamoja na “mjumbe wa agano” wake kwenye hekalu la kiroho, Yeye alipata mabaki wakiwa katika uhitaji wa kusafishwa na kutakaswa. Kwa mfano, Mnara wa Mlinzi, ulikuwa umewatia moyo wasomaji wao waweke kando siku ya Mei 30, 1918 kuwa siku ya sala kwa ajili ya ushindi wa mamlaka za kidemokrasi, kama ilivyokuwa imeagizwa na baraza kuu la U.S. na Rais Wilson. Jambo hili lilikuwa kuvunja kutokuwamo kwa Kikristo.​—Yohana 17:14, 16.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki