Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi—1991 | Mei 15
    • Hata hivyo, mengine ya yale ambayo Yesu alisema yalienea kupita safari ya kuhubiri ya mitume. Aliwaambia hivi: “Jihadharini na wanadamu; kwa maana watawapeleka mabarazani, na katika masinagogi yao watawapiga; nanyi mtachukuliwa mbele ya maliwali na wafalme kwa ajili yangu, kuwa ushuhuda kwao na kwa mataifa.” (Mathayo 10:17, 18) Katika safari hiyo, yaelekea wale 12 walikabili upinzani, lakini hakuna ushuhuda wowote kuonyesha kwamba walipelekwa “mbele ya maliwali na wafalme” kutoa ushuhuda kwa “mataifa.”a Katika miaka ya baadaye, mitume walienda mbele ya watawala, kama vile Wafalme Herode Agrippa I na II, Sergio Paulo, Galio, na hata Maliki Nero. (Matendo 12:1, 2; 13:6, 7; 18:12; 25:8-12, 21; 26:1-3) Kwa hiyo maneno ya Yesu yalikuwa na utumizi baadaye.

  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi—1991 | Mei 15
    • a Tafsiri nyinginezo zinafasiri hilo kuwa “wapagani” (The Jerusalem Bible), “Wasio Wayahudi” (New International Version na tafsiri za Moffatt na Lamsa), na “washenzi” (The New English Bible).

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki