-
Una Thamani Machoni pa Mungu!Amkeni!—1999 | Juni 8
-
-
Kwa mfano, akitoa kielezi cha thamani ya kila mmoja wa wanafunzi wake, Yesu alisema: “Je, shore wawili hawauzwi kwa sarafu ya thamani ndogo? Na bado hakuna hata mmoja wao atakayeanguka kwenye ardhi bila Baba yenu kujua. Lakini nywele zenyewe za kichwa chenu zimehesabiwa zote. Kwa hiyo msiwe na hofu: Nyinyi ni bora zaidi kuliko shore wengi.” (Mathayo 10:29-31) Fikiria maneno hayo yalimaanisha nini kwa wasikilizaji wa Yesu wa karne ya kwanza.
-
-
Una Thamani Machoni pa Mungu!Amkeni!—1999 | Juni 8
-
-
Je, unapata maana ya kielezi cha Yesu chenye kuchangamsha? Ikiwa Yehova huona hata ndege wadogo kuwa wenye thamani, lazima watumishi wake wa kidunia wawe wenye thamani hata zaidi kwake! Kila mmoja wetu ana thamani mbele za Yehova hata tunapokuwa miongoni mwa umati. Kila mmoja wetu ni mwenye thamani kwa Yehova hivi kwamba yeye hujua hata mambo madogo kutuhusu—nywele za vichwa vyetu zimehesabiwa zote.
-