Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Yesu Kristo
    Ufahamu wa Kina wa Maandiko
    • Kwa hiyo, pia, ni hakika kwamba wakati roho waovu walipoitii amri ya Yesu ya kutoka ndani ya watu waliopagawa, wao walifanya hivyo, si kwa msingi wa Yesu kuwa Mwana-Kondoo wa Mungu mwenye kutolewa dhabihu, bali ni kwa sababu ya mamlaka ambayo jina lake lilisimamia akiwa mwakilishi wa Ufalme aliyetiwa mafuta, mwenye mamlaka ya kuitisha, si kikosi kimoja tu, bali vikosi kumi na viwili vya malaika, vinavyoweza kufukuza roho waovu wowote ambao wangeweza kupinga kwa ushupavu agizo la kuondoka. (Mk 5:1-13; 9:25-29; Mt 12:28, 29; 26:53; linganisha Da 10:5, 6, 12, 13.) Mitume waaminifu wa Yesu walipewa mamlaka ya kulitumia jina lake kufukuza roho waovu, kabla na baada ya kifo chake pia. (Lu 9:1; 10:17; Mdo 16:16-18) Lakini wakati wana wa kuhani Myahudi Skewa walipojaribu kulitumia jina la Yesu katika njia hiyo, yule roho mwovu alitokeza kipingamizi kuwa wana haki gani ya kuitia mamlaka ambayo jina hilo liliwakilisha na kumfanya yule mwanamume aliyepagawa awashambulie na kuwararua.—Mdo 19:13-17.

  • Ufalme wa Mungu
    Ufahamu wa Kina wa Maandiko
    • Uwezo wa kifalme wa Yehova kuelekea uumbaji wake wa kidunia ulidhihirishwa kwa njia yenye kuonekana katika njia nyingi na Mwakilishi wake wa kifalme. Kwa roho ya Mungu, au nguvu ya utendaji, Mwanaye alidhibiti upepo na bahari, uoto, samaki, na hata visehemu vingine vilivyo ndani ya chakula, akisababisha chakula kiongezeke. Matendo hayo yenye nguvu yaliwafanya wanafunzi wasitawishe heshima yenye kina kwa ajili ya mamlaka aliyokuwa nayo. (Mt 14:23-33; Mk 4:36-41; 11:12-14, 20-23; Lu 5:4-11; Yoh 6:5-15) Hata jambo la kuvutia zaidi lilikuwa ni utumizi wake wa uwezo wa Mungu juu ya miili ya kibinadamu, akiponya maradhi kuanzia upofu hadi ukoma, na kuwarudisha wafu kwenye uzima. (Mt 9:35; 20:30-34; Lu 5:12, 13; 7:11-17; Yoh 11:39-47) Alituma wakoma walioponywa wakaripoti kwa makuhani, waliopewa mamlaka ya kimungu, lakini ambao kwa ujumla walikuwa wasioamini, ili iwe “ushahidi kwao.” (Lu 5:14; 17:14) Mwishowe, alionyesha uwezo wa Mungu juu ya roho wenye nguvu zinazopita zile kibinadamu. Roho waovu walitambua mamlaka aliyokuwa nayo Yesu na, badala ya kutaka mtihani wa makabiliano dhidi ya uwezo uliokuwa ukimuunga mkono, wao walikubali maagizo yake kwamba waachilie watu waliopagawa nao. (Mt 8:28-32; 9:32, 33; linganisha Yak 2:19.) Kwa kuwa ufukuzaji huo wa nguvu nyingi wa roho waovu ulifanywa kupitia roho ya Mungu, hilo lilimaanisha kwamba Ufalme wa Mungu ulikuwa kwa kweli “umewafikia” wasikilizaji wake.—Mt 12:25-29; linganisha Lu 9:42, 43.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki