Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kugeuka Sura​—Wamwona Yesu Katika Utukufu
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
    • Yesu akiwa anafundisha watu katika eneo la Kaisaria Filipi, ambalo liko karibu kilomita 25 hivi kutoka mlima Hermoni, anawatangazia mitume wake jambo lenye kushangaza: “Kwa kweli ninawaambia kwamba kuna baadhi ya wale waliosimama hapa ambao hawataonja kifo kamwe kabla ya kumwona Mwana wa binadamu akija katika Ufalme wake.”—Mathayo 16:28.

      Lazima wanafunzi wanajiuliza Yesu anamaanisha nini. Baada ya juma moja hivi, anawachukua watatu kati ya mitume wake—Petro, Yakobo, na Yohana—na kwenda kwenye mlima mrefu. Huenda ni usiku, kwa kuwa wanaume hao watatu wana usingizi. Yesu akiwa anasali, anageuka sura mbele yao. Mitume hao wanaona uso wake uking’aa kama jua. Na mavazi yake yakiwa maangavu kama nuru, yanakuwa meupe na kumetameta.

  • Kugeuka Sura​—Wamwona Yesu Katika Utukufu
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
    • Maono hayo yanamwimarisha sana Yesu na mitume wake! Yanaonyesha utukufu wa wakati ujao wa Kristo katika Ufalme. Kwa hiyo wanafunzi walimwona “Mwana wa binadamu akija katika Ufalme wake,” kama Yesu alivyoahidi. (Mathayo 16:28) Wakiwa mlimani, ‘walijionea kwa macho fahari yake.’ Ingawa Mafarisayo walitaka ishara ya kuthibitisha kwamba Yesu atakuwa Mfalme aliyechaguliwa na Mungu, hakuwapa ishara hata moja. Lakini wanafunzi wa karibu wa Yesu waliruhusiwa kuona kugeuka sura kwa Yesu, kunakothibitisha unabii kuhusu Ufalme. Hivyo, Petro angeweza kuandika hivi baadaye: “Tuna neno la kinabii likiwa limefanywa hakika zaidi.”—2 Petro 1:16-19.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki