Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Sikiliza Neno la Mungu la Kiunabii
    Mnara wa Mlinzi—2000 | Aprili 1
    • 5. Kwa maneno yako mwenyewe, ungefafanuaje mgeuko-umbo?

      5 Mgeuko-umbo ulikuwa tukio la kiunabii. Yesu alisema: “Mwana wa binadamu akusudiwa kuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake . . . Kwa kweli nawaambia nyinyi kwamba kuna baadhi ya wale ambao wamesimama hapa ambao hawataonja kifo hata kidogo mpaka kwanza wamwone Mwana wa binadamu akija katika ufalme wake.” (Mathayo 16:27, 28) Je, kweli baadhi ya mitume walimwona Yesu akija katika Ufalme wake? Mathayo 17:1-7 yasema: “Siku sita baadaye Yesu alichukua pamoja naye Petro na Yakobo na Yohana ndugu yake akawaleta juu katika mlima ulioinuka sana wakiwa peke yao wenyewe. Naye akageuka umbo mbele yao.” Ni tukio lenye kutokeza kama nini! “Uso wake ukang’aa kama jua, na mavazi yake ya nje yakawa maangavu kama nuru. Na, tazama! kukaonekana kwao Musa na Eliya, wakiongea naye.” Pia, “wingu jangavu liliwafunika kivuli,” wakasikia sauti ya Mungu mwenyewe ikisema: “‘Huyu ni Mwana wangu, mpendwa, ambaye mimi nimemkubali; msikilizeni yeye.’ Waliposikia hilo wanafunzi wakaanguka kifudifudi na kuwa wenye kuogopa sana. Ndipo Yesu akaja karibu na, akiwagusa, akasema: ‘Inukeni na msiwe na hofu.’”

  • Sikiliza Neno la Mungu la Kiunabii
    Mnara wa Mlinzi—2000 | Aprili 1
    • 7. Tunajuaje kwamba Petro aliukumbuka vizuri ule mgeuko-umbo?

      7 Huo mgeuko-umbo ulisaidia kuimarisha imani ya mitume hao watatu ambao wangekuwa na madaraka makubwa katika kutaniko la Kikristo. Uso wa Kristo wenye kung’aa kwa uangavu, mavazi yake meupe pe, na sauti ya Mungu mwenyewe ikitangaza kwamba Yesu ni Mwana Wake mpendwa wanayepaswa kumsikiliza—yote hayo yalitimiza ifaavyo kabisa kusudi la mgeuko-umbo. Lakini mitume hawakupaswa kumwambia mtu yeyote ono hilo mpaka Yesu afufuliwe. Miaka 32 baadaye, bado Petro alikumbuka vizuri ono hilo. Akilirejezea ono hilo na maana yake, aliandika: “Sivyo, haikuwa kwa kufuata hadithi zisizo za kweli zilizotungwa kwa usanifu mwingi kwamba tuliwafahamisha nyinyi juu ya nguvu na kuwapo kwa Bwana wetu Yesu Kristo, lakini ilikuwa kwa kupata kuwa mashahidi wa kujionea fahari yake. Kwa maana alipokea kutoka kwa Mungu Baba heshima na utukufu, wakati maneno ya namna hii yalipopelekwa kwake kwa utukufu wenye fahari: ‘Huyu ni mwana wangu, mpendwa wangu, ambaye mimi mwenyewe nimemkubali.’ Ndiyo, maneno haya tuliyasikia yakipelekwa kutoka mbinguni tulipokuwa tungali pamoja naye katika mlima mtakatifu.”—2 Petro 1:16-18.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki