-
Yehova Hutaka Nini Kutoka Kwetu Leo?Mnara wa Mlinzi—1999 | Septemba 15
-
-
3, 4. (a) Kwa ujumla, Yehova hutaka nini kutoka kwetu leo? (b) Kwa nini tuzifuate hatua za Yesu kwa ukaribu?
3 Katika mwaka wa mwisho wa huduma ya Yesu, mitume wake Petro, Yakobo, na Yohana waliandamana naye kwenye mlima mrefu, labda kilima kilichoko kwenye Mlima Hermoni. Huko waliona ono la unabii juu ya Yesu akiwa katika utukufu mkuu nao wakasikia sauti ya Mungu mwenyewe ikitangaza: “Huyu ni Mwana wangu, mpendwa, ambaye mimi nimemkubali; msikilizeni yeye.” (Mathayo 17:1-5) Kwa ujumla, Yehova hutaka haya kutoka kwetu—kumsikiliza Mwana wake na kufuata kielelezo na mafundisho yake. (Mathayo 16:24) Hivyo, mtume Petro aliandika hivi: “Kristo aliteseka kwa ajili yenu, akiwaachia kigezo ili nyinyi mfuate hatua zake kwa ukaribu.”—1 Petro 2:21.
-
-
Yehova Hutaka Nini Kutoka Kwetu Leo?Mnara wa Mlinzi—1999 | Septemba 15
-
-
5. Wakristo wako chini ya sheria gani, na sheria hiyo ilianza kutenda lini?
5 Kumsikiliza na kumwiga Yesu kwahusisha nini? Je, kwamaanisha kuwa chini ya sheria? Paulo aliandika hivi: “Mimi mwenyewe siko chini ya sheria.” Alikuwa akirejezea “agano la zamani,” agano la Sheria lililofanywa na Israeli. Paulo alikiri kwamba yupo “chini ya sheria kuelekea Kristo.” (1 Wakorintho 9:20, 21; 2 Wakorintho 3:14) Agano la Sheria la zamani lilipokoma, “agano jipya” likaanza kutenda likiwa na “sheria [yake] ya Kristo” ambayo watumishi wote wa Yehova leo huwajibika kuitii.—Luka 22:20; Wagalatia 6:2; Waebrania 8:7-13.
-