Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Sikiliza Neno la Mungu la Kiunabii
    Mnara wa Mlinzi—2000 | Aprili 1
    • 6. (a) Kwa nini Yesu aliuita mgeuko-umbo ono? (b) Mgeuko-umbo ulitangulia kuonyesha nini?

      6 Yamkini jambo hilo lenye kutia kicho lilitukia katika kilima kimoja kwenye Mlima Hermoni, ambako Yesu na mitume wake watatu walipisha usiku huo. Yaonekana kwamba mgeuko-umbo huo ulitukia usiku, jambo lililofanya uonekane dhahiri kabisa. Sababu moja iliyofanya Yesu aliite tukio hilo ono ni kwamba Musa na Eliya hawakuwepo kihalisi. Kristo peke yake ndiye aliyekuwapo kihalisi. (Mathayo 17:8, 9) Wonyesho huo mwangavu sana ulimpa Petro, Yakobo, na Yohana mwono wa kimbele wenye kutokeza wa kuwapo kwa Yesu kwenye utukufu katika uweza wa Ufalme. Musa na Eliya walifananisha warithi watiwa-mafuta wanaoshirikiana na Yesu, na ono hilo liliimarisha sana ushuhuda wake kuhusu Ufalme na utawala wake wa baadaye.

  • Sikiliza Neno la Mungu la Kiunabii
    Mnara wa Mlinzi—2000 | Aprili 1
    • 8. (a) Maneno ya Mungu kuhusu Mwana wake yalikazia nini? (b) Wingu lililotokea katika mgeuko-umbo lilionyesha nini?

      8 Jambo lililokuwa muhimu zaidi ni tangazo hili la Mungu: “Huyu ni Mwana wangu, mpendwa, ambaye mimi nimemkubali; msikilizeni yeye.” Taarifa hii yamkazia fikira Yesu akiwa Mfalme aliyetawazwa wa Mungu, ambaye uumbaji wote wapaswa kumtii. Wingu lililowafunika lilionyesha kwamba utimizo wa ono hilo haungeonekana. Ungetambuliwa tu kwa macho ya uelewevu ya wale wanaotambua “ishara” ya kuwapo kusikoonekana kwa Yesu katika mamlaka ya Ufalme. (Mathayo 24:3) Kwa hakika, maagizo ya Yesu kwamba wasimwambie mtu awaye yote ono hilo hadi afufuliwe kutoka katika wafu yaonyesha kwamba kukwezwa na kutukuzwa kwake kungetukia baada ya kufufuliwa kwake.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki