Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Wewe Husuluhishaje Matatizo?
    Mnara wa Mlinzi—1994 | Julai 15
    • Kusuluhisha Matatizo Makubwa

      “Na ndugu yako akikukosea, enenda ukamwonye, wewe na yeye peke yenu; akikusikia, umempata nduguyo. La, kama hasikii, chukua pamoja nawe tena mtu mmoja au wawili, ili kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno lithibitike. Na asipowasikiliza wao, liambie kanisa [“kutaniko,” NW]; na asiposikiliza kanisa pia, na awe kwako kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru.”—Mathayo 18:15-17.

      Vipi ikiwa Myahudi (au baadaye, Mkristo) angepata matatizo mazito baina yake na mwabudu wa Yehova mwenzake? Yule ambaye alifikiri kwamba amefanyiwa dhambi ndiye aliyepaswa kuchukua hatua ya kwanza. Angezungumzia mambo hayo pamoja na mkosaji kwa faragha. Akijaribu kutotetea upande wake, hakika ataelekea zaidi kupata ndugu yake, hasa kama tatizo lilikuwa ni kutoelewana ambako kungesuluhishwa kirahisi. Kila kitu kingesuluhishwa kwa urahisi zaidi ikiwa wale wanaohusika kwa njia ya moja kwa moja zaidi ndio watu pekee wanaojua habari hiyo.

  • Wewe Husuluhishaje Matatizo?
    Mnara wa Mlinzi—1994 | Julai 15
    • Uwezekano wa mtenda-kosa asiyetubu kutengwa na ushirika waonyesha kwamba Mathayo 18:15-17 halisemi juu ya matatizo madogo-madogo. Yesu alikuwa akirejezea makosa mazito, na ambayo yangesuluhishwa kati ya watu wawili wanaohusika. Kwa kielelezo, kosa laweza kuwa uchongezi, likiharibu kabisa sifa ya mchongewa. Au laweza kuhusika na mambo ya kifedha, kwa sababu mistari ifuatayo ina kielezi cha Yesu juu ya mtumwa mkatili aliyekuwa amesamehewa deni kubwa. (Mathayo 18:23-35) Mkopo usiolipwa kwa wakati uliotakikana waweza kuwa tu tatizo la muda liwezalo kusuluhishwa kati ya watu wawili. Lakini laweza kuwa dhambi nzito, yaani, wizi, ikiwa mwenye deni akataa kwa ukaidi kulipa deni lake.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki