-
Wewe Husuluhishaje Matatizo?Mnara wa Mlinzi—1994 | Julai 15
-
-
“Na ndugu yako akikukosea, enenda ukamwonye, wewe na yeye peke yenu; akikusikia, umempata nduguyo. La, kama hasikii, chukua pamoja nawe tena mtu mmoja au wawili, ili kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno lithibitike. Na asipowasikiliza wao, liambie kanisa [“kutaniko,” NW]; na asiposikiliza kanisa pia, na awe kwako kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru.”—Mathayo 18:15-17.
-
-
Wewe Husuluhishaje Matatizo?Mnara wa Mlinzi—1994 | Julai 15
-
-
Hata hivyo, huenda hatua ya kwanza isitoshe. Ili kushughulika na hali hiyo, Yesu alisema hivi: “Chukua pamoja nawe . . . mmoja au wawili.” Hao hasa waweza kuwa mashahidi waliojionea kisa hicho. Labda walisikia mmoja wa watu hao akichongea mwingine, au hata wale wanaochukuliwa walikuwa mashahidi wa mapatano yaliyoandikwa ambayo sasa watu hao wawili watofautiana juu yayo. Kwa upande mwingine, wale wanaochukuliwa wangekuwa mashahidi iwapo mambo yoyote, kama vile ushuhuda ulioandikwa au kusemwa kwa mdomo, yatokezwa kuthibitisha sababu ya tatizo. Hapa pia, ni idadi ndogo iwezekanavyo—“mmoja au wawili”—ndio wanaopaswa kujua jambo hilo. Jambo hilo lingefanya mambo yasiwe mabaya zaidi ikiwa tatizo lilikuwa ni kutoelewana tu.
Yule aliyekosewa apaswa kuwa na makusudi gani? Je! ajaribu kushusha heshima ya Mkristo mwenzake na kumtaka avunje heshima yake? Kwa kufikiria shauri la Yesu, Wakristo hawapaswi kuwa wepesi kushutumu ndugu zao. Mkosaji akitambua kosa lake, aombe msamaha, na ajaribu kurekebisha mambo, yule aliyetendewa dhambi atakuwa ‘amempata nduguye.’—Mathayo 18:15.
-
-
Wewe Husuluhishaje Matatizo?Mnara wa Mlinzi—1994 | Julai 15
-
-
Uwezekano wa mtenda-kosa asiyetubu kutengwa na ushirika waonyesha kwamba Mathayo 18:15-17 halisemi juu ya matatizo madogo-madogo. Yesu alikuwa akirejezea makosa mazito, na ambayo yangesuluhishwa kati ya watu wawili wanaohusika. Kwa kielelezo, kosa laweza kuwa uchongezi, likiharibu kabisa sifa ya mchongewa. Au laweza kuhusika na mambo ya kifedha, kwa sababu mistari ifuatayo ina kielezi cha Yesu juu ya mtumwa mkatili aliyekuwa amesamehewa deni kubwa. (Mathayo 18:23-35) Mkopo usiolipwa kwa wakati uliotakikana waweza kuwa tu tatizo la muda liwezalo kusuluhishwa kati ya watu wawili. Lakini laweza kuwa dhambi nzito, yaani, wizi, ikiwa mwenye deni akataa kwa ukaidi kulipa deni lake.
-