Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kuna Kosa Gani Kuwa na Wake Zaidi ya Mmoja?
    Amkeni!—1991 | Novemba 8
    • Kwa ndoa za Kikristo, Yesu alirudisha tena kiwango cha awali cha Mungu—kuoa mke mmoja tu. (Mathayo 19:4, 5) Zaidi ya hilo, alionyesha kwamba watu waliooa au kuolewa wapaswa kupatana sasa na takwa hilo la kimungu. Kama vile alivyoeleza: “Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe.” (Mathayo 19:6) Hivyo, Mkristo aliyeoa lazima alinde kifungo cha “mwili mmoja” ambacho huwa kati yake na mwenzi wake halali.b Kufanya ngono na mke aliye mtu wa tatu katika ndoa yako kungekuwa ni kuenda kinyume cha mpango huo wa kimungu. Kitendo kama hicho kimekatazwa katika kundi la Kikristo.—1 Wakorintho 5:11; 6:9, 16, 18; Waebrania 13:4.

  • Kuna Kosa Gani Kuwa na Wake Zaidi ya Mmoja?
    Amkeni!—1991 | Novemba 8
    • b The New International Dictionary of New Testament Theology yasema kwamba neno la Kigiriki lililotafsiriwa “mwili mmoja” katika Mathayo 19:5b lina maana ya kipekee kama ile tafsiri ya maneno ya Kiebrania ya Mwanzo 2:24 na humaanisha “ushirikiano kamili wa mwanamume na mwanamke ambao hauwezi kuvunjwa bila ya kuwaumiza washirika wenyewe.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki