-
UpendoAmkeni!—2018 | Na. 1
-
-
Yesu Kristo alifundisha kanuni muhimu sana za ndoa. Kwa mfano, alisema: “‘Mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye atashikamana na mke wake, na hao wawili watakuwa mwili mmoja’ . . . Kwa hiyo, kile ambacho Mungu ameunganisha mtu yeyote asikitenganishe.” (Mathayo 19:5, 6) Andiko hilo linatupatia kanuni mbili muhimu.
-
-
UpendoAmkeni!—2018 | Na. 1
-
-
“KILE AMBACHO MUNGU AMEUNGANISHA.” Ndoa pia ni muungano mtakatifu. Wenzi wanaotambua na kuheshimu ukweli huo hujitahidi kuimarisha ndoa yao. Hawatafuti njia za kuvunja ndoa yao matatizo yanapotokea. Upendo wao ni imara na thabiti. Upendo wa aina hiyo “huvumilia mambo yote,” na kuwachochea wenzi watatue matatizo yao ili kudumisha amani na umoja katika ndoa.
-