Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Wafanya Kazi Katika Shamba la Mizabibu
    Mnara wa Mlinzi—1989 | Agosti 15
    • Mwenye nyumba, au mwenye shamba la mizabibu, ni Yehova Mungu, nalo shamba la mizabibu ni taifa la Israeli. Wafanya kazi katika shamba la mizabibu ni watu walioingizwa katika agano la Sheria; wao hasa ni wale Wayahudi wenye kuishi siku za mitume. Patano la kutoa mshahara hufanywa pamoja na wafanya kazi wa mchana mzima tu. Mshahara ule ni dinari moja kwa kazi ya mchana ule. Kwa kuwa “saa tatu” ni saa 3:00 ya asubuhi, wale walioitwa wakati wa saa 3, saa 6, saa 9, na saa 11 hufanya kazi kwa muda wa saa 9, 6, 3, na 1 tu.

      Wafanya kazi wa muda wa saa 12, au mchana mzima, wawakilisha viongozi Wayahudi ambao wamekuwa wakiendelea kujishughulisha sana katika utumishi wa kidini. Wao si kama wanafunzi wa Yesu, ambao kwa sehemu kubwa ya maisha zao wamekuwa wameajiriwa kuvua samaki au katika shughuli nyinginezo za kimwili. Ilipofika vuli ya 29 W.K., hapo tu ndipo “mwenye nyumba” alipomtuma Yesu Kristo akawakusanye hawa kuwa wanafunzi wake. Hivyo wakawa “wa mwisho,” au wafanya kazi wa saa 11 katika shamba la mizabibu.

  • Wafanya Kazi Katika Shamba la Mizabibu
    Mnara wa Mlinzi—1989 | Agosti 15
    • Kupokea dinari zile hakukutukia kwenye kifo cha Yesu, bali kwenye Pentekoste 33 W.K., wakati ambapo Kristo, yule “msimamizi,” alimimina roho takatifu juu ya wanafunzi wake. Wanafunzi hawa wa Yesu walikuwa kama watu wale “wa mwisho,” au wafanya kazi wa saa 11.

  • Wafanya Kazi Katika Shamba la Mizabibu
    Mnara wa Mlinzi—1989 | Agosti 15
    • Je! utimizo huo wa karne ya kwanza ndio utimizo wa pekee wa kielezi cha Yesu? Hapana, kwa sababu ya vyeo na madaraka yao, makasisi wa Jumuiya ya Wakristo katika karne hii ya 20 wamekuwa “wa kwanza” kuajiriwa kazi katika shamba la mizabibu la Mungu lililo la ufananisho. Wao waliwachukua wahubiri waliojiweka wakfu wenye kushirikiana na Sosaiti ya Mnara wa Mlinzi Biblia na Trakti kuwa “wa mwisho” kupata mgawo wowote halali katika utumishi wa Mungu. Lakini, kwa uhakika, watu hawa hawa ambao makasisi waliwadharau ndio walioipokea dinari —ile heshima ya kutumikia wakiwa mabalozi wapakwa-mafuta wa Ufalme wa kimbingu wa Mungu. Mathayo 19:30–20:16.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki