-
Wafanya Kazi Katika Shamba la MizabibuMnara wa Mlinzi—1989 | Agosti 15
-
-
Mwishowe, siku ya kazi ya ufananisho yafikia mwisho na kifo cha Yesu, na wakati waja wa kuwalipa wafanya kazi. Kanuni isiyo ya kawaida ya kuwalipa kwanza walio wa mwisho yafuatwa, kama ielezwavyo: “Kulipokuchwa, yule bwana wa shamba akamwambia msimamizi wake, Waite wakulima, uwalipe ujira wao, ukianzia wa mwisho hata wa kwanza. Na walipokuja wale wa saa kumi na moja, walipokea kila mtu dinari. Na wale wa kwanza walipokuja, walidhani kwamba watapokea zaidi; na hao pia wakapokea kila mtu dinari. Basi wakiisha kuipokea, wakamnung’unikia mwenye nyumba, wakisema, Hao wa mwisho wametenda kazi saa moja tu, nawe umewasawazisha na sisi tuliostahimili taabu na hari za mchana kutwa. Naye akamjibu mmoja wao, akamwambia, Rafiki, sikudhulumu; hukupatana nami kwa dinari? Chukua iliyo yako, uende zako; napenda kumpa huyu wa mwisho sawa na wewe. Si halali yangu kutumia vilivyo vyangu kama nipendavyo? Au jicho lako limekuwa ovu kwa sababu ya mimi kuwa mwema?” Kwa kumalizia Yesu alirudia jambo lililotajwa mapema akisema hivi: “Vivyo hivyo wa mwisho watakuwa wa kwanza, na wa kwanza watakuwa wa mwisho.”
-
-
Wafanya Kazi Katika Shamba la MizabibuMnara wa Mlinzi—1989 | Agosti 15
-
-
Muda si muda wale walioajiriwa kwanza waliona kwamba wanafunzi wa Yesu walikuwa wamelipwa, na wakawaona wakiitumia dinari ya ufananisho. Lakini wao walitaka mengi zaidi ya roho takatifu na mapendeleo ya Ufalme yaliyoshirikishwa nayo. Kunung’unika kwao na vitendo vyao vya kukinza vilikuwa vya namna ya kunyanyasa wanafunzi wa Kristo, walio wafanya kazi “wa mwisho” katika shamba la mizabibu.
Je! utimizo huo wa karne ya kwanza ndio utimizo wa pekee wa kielezi cha Yesu? Hapana, kwa sababu ya vyeo na madaraka yao, makasisi wa Jumuiya ya Wakristo katika karne hii ya 20 wamekuwa “wa kwanza” kuajiriwa kazi katika shamba la mizabibu la Mungu lililo la ufananisho. Wao waliwachukua wahubiri waliojiweka wakfu wenye kushirikiana na Sosaiti ya Mnara wa Mlinzi Biblia na Trakti kuwa “wa mwisho” kupata mgawo wowote halali katika utumishi wa Mungu. Lakini, kwa uhakika, watu hawa hawa ambao makasisi waliwadharau ndio walioipokea dinari —ile heshima ya kutumikia wakiwa mabalozi wapakwa-mafuta wa Ufalme wa kimbingu wa Mungu. Mathayo 19:30–20:16.
-