-
Kafichuliwa na Vielezi vya Shamba la MizabibuMnara wa Mlinzi—1990 | Januari 1
-
-
“Mtu mmoja alikuwa na watoto wawili,” Yesu asimulia. “Akiendea yule wa kwanza, akasema, ‘Mtoto, enda ukafanye kazi leo katika shamba la mizabibu.’ Kwa kujibu huyu akasema, ‘Nitaenda, bwana,’ lakini hakwenda. Akikaribia yule wa pili, akasema ivyo hivyo. Kwa kujibu huyu akasema, ‘Mimi sitaenda.’ Baadaye akahisi majuto na kwenda. Ni yupi wa wale wawili aliyefanya penzi la baba yake?” Yesu auliza.
-
-
Kafichuliwa na Vielezi vya Shamba la MizabibuMnara wa Mlinzi—1990 | Januari 1
-
-
Kwa hiyo Yesu aeleza hivi: “Kwa kweli mimi nasema kwa nyinyi kwamba wakusanya-kodi na makahaba wanaenda mbele ya nyinyi kuingia katika ufalme wa Mungu.” Kwa kweli, wakusanya-kodi na makahaba walikataa kutumikia Mungu hapo kwanza. Lakini ndipo, kama yule mtoto wa pili, wakatubu na kumtumikia. Kwa upande mwingine, viongozi wa kidini, kama yule mtoto wa kwanza, walijidai kuwa watumikia Mungu, hata hivyo, kama vile Yesu aarifuvyo: “Yohana [Mbatizaji] alijia nyinyi katika njia ya uadilifu, lakini nyinyi hamkumwamini. Hata hivyo, wakusanya-kodi na makahaba walimwamini, na nyinyi, ingawa mliona jambo hili, hamkuhisi majuto baadaye ili mmwamini.”
-