Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ufalme wa Mungu Umeanza Kutawala!
    Furahia Maisha Milele!—Masomo ya Kujifunza Biblia
    • 2. Tangu mwaka wa 1914, hali zimekuwaje na watu wamekuwa wakitendaje?

      Wanafunzi wa Yesu walimwuliza hivi: “Ni nini itakayokuwa ishara ya kuwapo kwako na ya umalizio wa mfumo wa mambo?” (Mathayo 24:3) Yesu aliwajibu kwa kutabiri mambo mengi ambayo yangetokea wakati ambapo angeanza kutawala mbinguni akiwa Mfalme wa Ufalme wa Mungu. Baadhi ya mambo aliyotaja ni vita, upungufu wa chakula, na matetemeko ya ardhi. (Soma Mathayo 24:7.) Pia, Biblia ilitabiri kwamba tabia za watu katika “siku za mwisho” zingefanya hali ziwe “ngumu kushughulika nazo.” (2 Timotheo 3:1-5) Hali na tabia hizo zimeonekana waziwazi hasa tangu mwaka wa 1914.

      3. Kwa nini hali zimekuwa mbaya sana tangu Ufalme wa Mungu ulipoanza kutawala?

      Muda mfupi baada ya kuwa Mfalme wa Ufalme wa Mungu, Yesu alipigana vita mbinguni dhidi ya Shetani na roho waovu. Shetani alishindwa katika vita hivyo. Biblia inasema: “[alitupwa] chini duniani, na malaika zake wakatupwa chini pamoja naye.” (Ufunuo 12:9, 10, 12) Shetani ana hasira kali kwa sababu anajua kwamba ataangamizwa. Kwa hiyo, anasababisha maumivu na kuteseka ulimwenguni pote. Ndiyo sababu hali ni mbaya sana ulimwenguni! Ufalme wa Mungu utaondoa matatizo hayo yote.

  • Ufalme wa Mungu Umeanza Kutawala!
    Furahia Maisha Milele!—Masomo ya Kujifunza Biblia
    • 5. Ulimwengu umebadilika tangu mwaka wa 1914

      Onyesha VIDEO.

      VIDEO: Ulimwengu Umebadilika Tangu Mwaka wa 1914 (1:10)

      Yesu alitabiri kuhusu hali ambazo zingekuwa ulimwenguni wakati ambapo angeanza kutawala. Soma Luka 21:9-11, kisha mzungumzie swali hili:

      • Umesikia au kujionea nini kati ya mambo hayo yaliyotabiriwa?

      Mtume Paulo alifafanua jinsi ambavyo watu wangetenda wakati wa siku za mwisho za utawala wa wanadamu. Soma 2 Timotheo 3:1-5, kisha mzungumzie swali hili:

      • Umejionea watu wakiwa na tabia gani kati ya tabia hizo?

      Picha: Picha zinazoonyesha hali za ulimwengu na tabia za watu katika siku za mwisho. 1. Kiongozi wa jeshi akihutubu jukwaani kwa sauti kubwa akiwa ameinua mikono. 2. Majengo yaliyobomoka baada ya tetemeko la ardhi. 3. Ndege za vita. 4. Watu waliovaa barakoa wakitembea. 5. Majengo mawili jijini New York yanawaka moto baada ya shambulizi la kigaidi. 6. Mwanamume akitumia dawa za kulevya. 7. Mume akiwa amekunja ngumi akimgombeza mke wake. 8. Pombe na dawa mbalimbali za kulevya. 9. Wanawake wawili waliovaa mavazi ya kisasa na mapambo ya thamani wakijipiga picha. 10. Mtumbuizaji anatumbuiza umati wa watu. 11. Mwandamanaji akirusha bomu la petroli.
Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki