-
Ile Ishara Wewe Unaitii?Mnara wa Mlinzi—1988 | Oktoba 15
-
-
Wakati huo ulio wa maana kubwa sana uwasilipo, msimamo wako wewe utakuwa nini? Je! wewe utaachwa uwe wa uharibifu, au wewe utatwaliwa kwa ajili ya wokovu? Kukuongoza katika mwelekezo unaofaa, fikiria kielezi ambacho Yesu alitoa: “Po pote ulipo mzoga, ndipo watakapokusanyika tai [pamoja, NW].”—Luka 17:34-37; Mathayo 24:28.
Hivyo Yesu alikazia uhitaji wa kitendo cha kuona mbali, chenye muungamano. Wale wanaotwaliwa kwa ajili ya wokovu ni wale ambao hukusanyika pamoja kwa ukawaida na kunufaika kutokana na ulishaji wa kiroho ambao Mungu anaandaa. Mamilioni wamejionea kwamba malisho hayo ya kiroho yanakuja kupitia ushirika wa ukaribu pamoja na moja la makundi zaidi ya 55,000 ya Mashahidi wa Yehova na kupitia kujifunza vichapo vyenye msingi wa Biblia kama kile ambacho wewe unasoma sasa.
-
-
Tai Ndege-Wanofua-MizogaMnara wa Mlinzi—1988 | Oktoba 15
-
-
Tai Ndege-Wanofua-Mizoga
Ile Ishara
“PO POTE ulipo mzoga, ndipo watakapokusanyika tai [pamoja, NW].’ (Mathayo 24:28) Badala ya kujifunza somo kutokana na kielezi hicho, watu fulani wanatafuta-tafuta makosa ndani yacho. Wao wanasema kwamba tai ni wawindaji ambao hujiendea wakiwa peke yao na kujilisha mawindo yaliyo hai, si mizoga. Hivyo, Biblia fulani zinatumia neno “ndege-wanofua-mizoga.” Lakini neno la Kigiriki linalohusika, a·e·tosʹ, limetafsiriwa “tai” kama ifaavyo.
Jamii moja inayopatikana katika Israeli ni yule tai mwenye rangi ya kihudhurungi. “Kama ndege wengi wa mawindo,” wanaonelea John Sinclair na John Mendelsohn, “tai wa hudhurungi si asiyependa kula mizoga na mara nyingi sana anakuwa miongoni mwa walio wa kwanza kuwasili kwenye windo lililouawa hivi sasa tu.” Mwoneleaji mwingine anaripoti kikusanyiko cha tai 60 wa mikia mifupi na tai wa hudhurungi katika jangwa Kalahari la Afrika. Yeye aliongezea hivi: “Yule Tai Hudhurungi ndiye hutawala wengine wanapokutana penye mzoga. Katika visa kadhaa ndege wawili, wenye kudhaniwa kuwa mume na mkeye, wameonekana wakishirikiana kula windo lililouawa.”
Tai wa baharini wanapatikana sana pia katika mabara ya Mediterania. Katika karne zilizopita, tai wa baharini na tai wa bara walijilisha mizoga ya farasi waliochinjwa katika pigano. “Inajulikana vizuri . . . kwamba wao hufuata majeshi kwa kusudi hilo,” inataarifu Cyclopædia ya McClintock na Strong.
Kwa kuwa wana mwendo mwepesi sana na huona mbali, nyakati fulani tai huwa ndio ndege wa kwanza kuwasili kwenye mzoga uliouawa sasa hivi. Yesu aliifahamu sana ile fasili ambamo Yehova Mungu aliuliza Ayubu swali hili la kunyenyekeza: “Je! tai hupaa juu kwa amri yako, na kufanya kioto chake mahali pa juu . . . ya genge la jabali, na [mahali pasipoingilika, NW] ngomeni. Toka huko yeye huchungulia mawindo; macho yake huyaangalia toka mbali . . . Na kwenye maiti ndiko aliko.”—Ayubu 39:27-30.
Hivyo, Yesu alitoa vizuri kielezi cha kwamba ni wale tu wenye jicho la kitamathali lililo kama la tai ambao wangenufaika kutokana na ile ishara.
-