-
Ni Nini Hukuchochea Kumtumikia Mungu?Mnara wa Mlinzi—1995 | Juni 15
-
-
17. Katika maneno yako mwenyewe, eleza kifupi mfano wa talanta.
17 Ebu fikiria mfano wa Yesu wa talanta, kama ulivyorekodiwa kwenye Mathayo 25:14-30. Mtu mmoja aliyekuwa karibu kusafiri mbali aliwaita watumwa wake na kuwapa mali zake. “Akampa mmoja talanta tano, na mmoja talanta mbili, na mmoja talanta moja; kila mtu kwa kadiri ya uwezo wake.” Bwana-mkubwa aliporudi kutoza hesabu watumwa wake, alipata nini? Mtumwa aliyekuwa amepewa talanta tano alipata talanta tano zaidi. Vivyo hivyo, mtumwa aliyekuwa amepewa talanta mbili alipata talanta mbili zaidi. Mtumwa aliyekuwa amepewa talanta moja aliizika ardhini naye hakufanya lolote ili kuongeza mali ya bwana-mkubwa wake. Bwana-mkubwa alichanganuaje hali hiyo?
-
-
Ni Nini Hukuchochea Kumtumikia Mungu?Mnara wa Mlinzi—1995 | Juni 15
-
-
19 Bila shaka, mtumwa wa tatu hakupongezwa. Hata alitupwa katika giza la nje. Baada ya kupokea talanta moja tu, yeye hakutazamiwa kutokeza talanta nyingi kama yule mtumwa mwenye talanta tano. Lakini, yeye hata hakujaribu! Alipewa hukumu ya adhabu kwa sababu ya mtazamo wa moyo wake ulio “mbaya na ulegevu,” ulioonyesha ukosefu wa upendo kwa bwana-mkubwa.
-