-
“Basi, Nendeni Mkafanye Wanafunzi”Mnara wa Mlinzi (Funzo)—2020 | Januari
-
-
1-2. Malaika anawaambia nini wanawake waliofika kwenye kaburi la Yesu, naye Yesu anawapatia maagizo gani?
NI ASUBUHI na mapema, Nisani 16, 33 W.K. Kikundi chenye huzuni cha wanawake wanaomwogopa Mungu kinaelekea kwenye kaburi ambalo mwili wa Bwana Yesu Kristo ulizikwa zaidi ya saa 36 zilizopita. Wanapofika kaburini wakiwa na kusudi la kuupaka mwili wa Yesu manukato na mafuta yenye marashi, wanashangaa kukuta kaburi likiwa tupu! Malaika anawaambia wanafunzi hao kwamba Yesu amefufuliwa kutoka kwa wafu, na kuongezea hivi: “Anawatangulia kwenda Galilaya. Mtamwona huko.”—Mt. 28:1-7; Luka 23:56; 24:10.
-
-
“Basi, Nendeni Mkafanye Wanafunzi”Mnara wa Mlinzi (Funzo)—2020 | Januari
-
-
4 Yesu anataka wafuasi wake wote wahubiri. Hakuwapa amri hiyo wale mitume wake 11 waaminifu peke yao. Kwa nini tuna uhakika huo? Je, ni mitume peke yao waliokuwepo wakati amri ya kufanya wanafunzi ilipotolewa kwenye mlima huko Galilaya? Kumbuka kwamba malaika aliwaambia hivi wanawake hao: “Mtamwona huko [Galilaya].” Hivyo, hapana shaka kwamba wanawake hao waaminifu walikuwepo katika mkutano huo. Na si hivyo tu. Mtume Paulo anafunua kwamba Yesu “aliwatokea ndugu zaidi ya 500 kwa wakati mmoja.” (1 Kor. 15:6) Wapi?
-