Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Roho Takatifu—Kani ya Utendaji ya Mungu
    Je, Uamini Utatu?
    • Kwenye Mathayo 28:19, NW, rejezo hufanywa kwa “jina . . . la roho takatifu.” Lakini neno “jina” halimaanishi sikuzote jina la kibinafsi, ama katika Kigiriki ama katika Kiswahili. Tusemapo “katika jina la sheria,” hatuwi tunarejezea mtu. Huwa twamaanisha jambo lile ambalo sheria yasimamia, mamlaka yayo. Word Pictures in the New Testament ya Robertson husema hivi: “Katika Septuagint na mafunjo ni jambo la kawaida kutumia jina (onoma) hapa kwa kusema nguvu au mamlaka.” Kwa hiyo ubatizo ‘katika jina la roho takatifu’ hutambua mamlaka ya roho, ambayo hutoka kwa Mungu na hutenda kazi kwa mapenzi ya kimungu.

  • Namna Gani Juu ya “Maandiko-Ithibati” ya Utatu?
    Je, Uamini Utatu?
    • NEW Catholic Encyclopedia hutoa matatu ya hayo “maandiko-ithibati” lakini hukiri hivi pia: “Fundisho la Utatu Mtakatifu halifundishwi katika A[gano la] K[ale]. Katika A[gano] J[ipya] uthibitisho wa zamani kabisa umo katika nyaraka za Kipaulo, hasa 2 Kor 13.13 [mstari 14 katika Biblia fulani-fulani], na 1 Kor 12.4-6. Mahali dhahiri kabisa ambapo uthibitisho wa Utatu hupatikana katika zile Gospeli ni katika ile imani ya kiubatizo ya Mt 28.19.”

      Katika mistari hiyo wale “watu” watatu huorodheshwa ifuatavyo katika The New Jerusalem Bible. Wakorintho wa Pili 13:13 (14) huwaweka wote watatu pamoja kwa njia hii: “Neema ya Bwana Yesu Kristo, upendo wa Mungu na ushirika wa Roho Mtakatifu uwe pamoja na nyinyi nyote.” Wakorintho wa Kwanza 12:4-6 husema hivi: “Kuna zawadi tofauti nyingi, lakini sikuzote ni Roho yule yule; kuna njia tofauti nyingi za kutumikia, lakini sikuzote ni Bwana yule yule. Kuna namna tofauti nyingi za utendaji, lakini katika kila mtu ni Mungu yule yule mwenye kufanya kazi katika wote.” Na Mathayo 28:19 husomeka hivi: “Kwa hiyo, endeni mfanye wanafunzi wa mataifa yote; wabatizeni katika jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu.”

      Je! mistari hiyo husema kwamba Mungu, Kristo, na roho takatifu huwa muundo mmoja wa Uungu wa Utatu, kwamba kuna watatu wenye usawa wa asili, nguvu, na umilele? Sivyo, kama vile kuorodhesha watu watatu, kama Tom, Dick, na Harry, kusivyomaanisha kwamba wao ni watatu katika mmoja.

      Rejezo la namna hii, yakiri Cyclopedia of Biblical, Theological, and Ecclesiastical Literature ya McClintock na Strong, “huthibitisha tu kwamba kuna watu watatu wenye kutajwa jina, . . . lakini jambo hilo lenyewe tu halithibitishi kwamba wote watatu kwa lazima ni wa asili ya kimungu, na wana heshima sawa ya kimungu.”

      Ingawa chanzo hicho huunga mkono Utatu, chasema hivi juu ya 2 Wakorintho 13:13 (14): “Hatungeweza kukata shauri kwamba wao wana mamlaka yenye usawa, wala asili ile ile.” Nacho husema hivi juu ya Mathayo 28:18-20: “Hata hivyo, andiko hili likichukuliwa pekee, halingethibitisha kwa kukata maneno utu wa watu watatu wanaotajwa, wala usawa wala uungu wao.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki