Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Iweni Watendaji wa Neno, Si Wasikiaji Tu
    Mnara wa Mlinzi—1990 | Oktoba 1
    • 3. Ni agizo gani juu ya kuhukumu ambalo Yesu atoa halafu katika yale Mahubiri juu ya Mlima?

      3 Kadiri Yesu alivyoendelea na Mahubiri yake juu ya Mlima, semi zaidi ziliongezeka ambazo ni lazima Wakristo wajitahidi kufuata. Hapa pana mmoja uonekanao kuwa sahili, lakini washutumu moja la maelekeo yaliyo magumu kabisa kuondolea mbali: “Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi. Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa. Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huiangalii? Au utamwambiaje nduguyo, Niache nikitoe kibanzi katika jicho lako; na kumbe! mna boriti ndani ya jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako.”—Mathayo 7:1-5.

  • Iweni Watendaji wa Neno, Si Wasikiaji Tu
    Mnara wa Mlinzi—1990 | Oktoba 1
    • 5. Kwa nini ni rahisi zaidi kuona dosari katika wengine kuliko zile zilizo katika sisi wenyewe?

      5 Wakati wa karne ya kwanza W.K., kwa sababu ya mapokeo ya mdomo, Mafarisayo kwa ujumla walielekea kuhukumu wengine vikali. Wowote wa wasikilizaji wa Yesu waliokuwa katika zoea la kufanya hivyo walipaswa kulikomesha. Ni rahisi zaidi kuona kibanzi katika macho ya wengine kuliko maboriti yaliyo katika macho yetu wenyewe—tena kufanya hivyo kwatuongezea uhakika ili tujione! Kama alivyosema mwanamume mmoja, “Mimi napenda kuchambua wengine kwa sababu hiyo hunifanya nihisi vizuri sana!” Tabia ya kuchambua-chambua wengine huenda ikatupa sisi hisia za wema zionekanazo ni kama zasawazisha makosa yetu wenyewe tutakayo kuyaficha. Lakini ikiwa sahihisho ni la lazima, lapasa kutolewa kwa roho ya upole. Mwenye kutoa sahihisho apaswa kukumbuka wakati wote mapungukio yake mwenyewe.—Wagalatia 6:1.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki