Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi—1990 | Machi 15
    • Maswali Kutoka kwa Wasomaji

      ◼ Je! yatupasa tukate shauri kutokana na Mathayo 7:13, 14 na Luka 13:24 kwamba hata katika ufufuo, wanadamu walio wengi watakataa ibada ya kweli?

      Sivyo, mistari hii haiungi mkono kukata shauri jinsi hiyo. Bali, yahusu hasa kupata uhai katika Ufalme wa kimbingu.

      Maneno ya Yesu kwenye Mathayo 7:13, 14 ni sehemu ya Mahubiri ya Mlimani. Yeye alisema: “Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo. Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.”

      Mengi ya yale ambayo Yesu alisema katika pindi hii yalihusu hasa Ufalme wa kimbingu. Kwa kielelezo, yeye alianza kwa maneno haya: “Wenye furaha ni wale wenye kujua uhitaji wao wa kiroho, kwa kuwa ufalme wa mbingu ni wao.” Alisema kwamba wenye kutakata katika moyo ‘wangeona Mungu’ na kwamba “ufalme wa mbingu” ni wa wale “wenye kunyanyaswa kwa ajili ya uadilifu.” (Mathayo 5:3, 8, 10, NW) Baadaye katika hotuba iyo hiyo, Yesu alinena juu ya barabara pana inayoongoza kuingia katika uharibifu na barabara iliyosonga inayoongoza kwenye uhai. Kwa sehemu, aliongezea hivi: “Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.”—Mathayo 7:13, 14, 21.

  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi—1990 | Machi 15
    • Kwa hiyo, twaweza kuona kutokana na habari zenye kuzunguka vituko vyote viwili kwamba maelezo ya Yesu (juu ya kuwa kwa wachache katika barabara iliyosonga inayoongoza kwenye uhai na kuokolewa kwao) yalihusu hasa kuwa na kibali cha Mungu wakati huo ambapo Yeye alikuwa akitoa tumaini la uhai wa kimbingu. Waliosikia ujumbe wa ukweli na kujifunza yaliyotakwa na kuitikia wakathibitika kuwa waaminifu ni wachache kwa ulinganisho.— Mathayo 22:14; 24:13; Yohana 6:60-66.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki