-
Ona Mema kwa Ajili ya Kazi Yako Ngumu“Jitunzeni Katika Upendo wa Mungu”
-
-
6, 7. Ni nini kinachoonyesha kwamba Yesu amekuwa akifanya kazi kwa bidii kwa muda mrefu?
6 Yesu amekuwa akifanya kazi kwa bidii kwa muda mrefu. Kabla ya kuja duniani, alikuwa “stadi wa kazi” wa Mungu katika uumbaji wa vitu vyote “mbinguni na duniani.” (Methali 8:22-31; Wakolosai 1:15-17) Alipokuwa duniani, Yesu aliendelea kufanya kazi kwa bidii. Mapema katika maisha yake, alijifunza kazi ya ujenzi na akajulikana kuwa “seremala.”a (Marko 6:3) Useremala ni kazi ngumu na inahitaji ustadi mwingi, na ilikuwa hivyo hasa kabla ya kuwapo kwa viwanda vya kupasua mbao, maduka ya kuuza vifaa, na vifaa vinavyotumia umeme. Wazia Yesu akienda kutafuta mbao, labda hata kukata miti na kuburuta magogo mpaka mahali pake pa kazi! Wazia akijenga nyumba, akitengeneza na kuweka mbao za paa, milango, na hata fanicha! Bila shaka, Yesu mwenyewe alipata uradhi kwa kufanya kazi ngumu na kwa ustadi.
-
-
Ona Mema kwa Ajili ya Kazi Yako Ngumu“Jitunzeni Katika Upendo wa Mungu”
-
-
a Inasemekana kwamba neno la Kigiriki linalotafsiriwa “seremala” ni “neno la jumla linalotumiwa kumrejelea mtu anayefanya kazi ya kutengeneza vitu kwa kutumia mbao iwe ni nyumba, fanicha, au vifaa vingine vya mbao.”
-