Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Wanawake Wakristo Wastahili Heshima na Staha
    Mnara wa Mlinzi—1995 | Julai 15
    • 10 Kuhusu talaka, Yesu aliulizwa swali hili: “Je! ni halali mtu kumwacha [“kutaliki,” NW] mkewe kwa kila sababu?” Kulingana na simulizi la Marko, Yesu alisema hivi: “Yeyote yule atalikiye mke wake [isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati] na kuoa mwingine afanya uzinzi dhidi ya mke, na ikitukia wakati wowote mwanamke, baada ya kutaliki mume wake, aolewa na mwingine, yeye afanya uzinzi.” (Marko 10:10-12, NW; Mathayo 19:3, 9) Maneno hayo yenye kusemwa kwa usahili yalionyesha staha kwa heshima ya wanawake. Jinsi gani?

  • Wanawake Wakristo Wastahili Heshima na Staha
    Mnara wa Mlinzi—1995 | Julai 15
    • 12. Kwa maneno “afanya uzinzi dhidi ya mke,” Yesu alikuwa akitoa wazo jipi?

      12 Pili, kwa maneno “afanya uzinzi dhidi ya mke,” Yesu alitoa maoni ambayo hayakutambuliwa katika mahakama za kirabi—wazo la mwanamume kufanya uzinzi dhidi ya mkeye. The Expositor’s Bible Commentary yaeleza hivi: “Katika Dini ya Kiyahudi ya kirabi mwanamke angeweza kufanya uzinzi dhidi ya mume wake kwa kutokuwa mwaminifu; na mwanamume, kwa kufanya ngono na mke wa mwanamume mwingine, angeweza kufanya uzinzi dhidi ya mume huyo. Lakini mwanamume asingeweza kamwe kufanya uzinzi dhidi ya mke wake, hata awe amefanya nini. Yesu aliinua hali na heshima ya wanawake, kwa kumweka mume chini ya wajibu uleule wa kiadili kama mke.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki