Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Wazazi Fikieni Moyo wa Mtoto Wenu Kutoka Utoto Mchanga
    Mnara wa Mlinzi—1988 | Agosti 1
    • 1. Ni jambo gani lililotukia wakati wa kipindi kimoja chenye majaribu sana katika maisha ya Yesu?

      YESU KRISTO na wanafunzi wake walikuwa njiani kwenda Yerusalemu. Si muda mrefu kabla ya hapo, katika pindi mbili tofauti-tofauti, Yesu alikuwa ameambia wanafunzi wake kwamba yeye angepita chini ya mateso mengi na kuuawa katika jiji hilo. (Marko 8:31; 9:31) Wakati wa kipindi hiki chenye kumjaribu sana Yesu, usimulizi wa Biblia unasema: “Watu walianza kumletea pia vitoto vichanga vyao ili aguse hivi.”​—Luka 18:15, NW.

      2. (a) Huenda ikawa ni kwa nini wanafunzi walijaribu kuambia watu waende zao? (b) Yesu aliitikiaje hali hiyo?

      2 Jibu lilikuwa nini kwa jambo hili? Basi, wanafunzi waligombeza wale watu na kujaribu kuwaondosha waende zao, bila shaka wakiitikadi kwamba wao walikuwa wakifanyia Yesu hisani kwa kumpa himaya asipatwe na sumbuo na mfinyo usiohitajiwa kabisa. Lakini Yesu akawa mwenye ghadhabu kwa wanafunzi wake, akisema: “‘Acheni watoto wachanga waje kwa mimi; msijaribu kuwakomesha’ . . . Na yeye akachukua wale watoto ndani ya mikono yake na kuanza kuwabariki.” (Marko 10:13-16, NW) Ndiyo, zijapokuwa fikira zote ambazo bila shaka zilikuwa zimekuwa katika akili na moyo wake, Yesu alichukua wakati wa kuwa na vitoto vichanga.

  • Wazazi Fikieni Moyo wa Mtoto Wenu Kutoka Utoto Mchanga
    Mnara wa Mlinzi—1988 | Agosti 1
    • 9. Watoto wanahitaji kupewa himaya wasipatwe na uchafuzi gani?

      9 Hata hivyo, kwa sababu ya mkazo wa nyakati hizi ambamo sisi tunaishi, huenda wewe ukawa na mbetuko, kama ule ambao wanafunzi walikuwa nao, wa kugeuzia watoto kando ili wewe uweze kuhudumia ile ambayo huenda ikawaziwa kuwa ndiyo kazi iliyo ya maana zaidi. Lakini ni nini kilicho cha maana kuliko watoto wako mwenyewe? Maisha zao za kiroho zimo hatarini! Huenda wewe ukawa unakumbuka kwamba wakati ile aksidenti ya nyukilia kule Chernobyl ilipotukia katika Urusi katika 1986 watoto waliondolewa kwenye jimbo hilo ili kuwahami na uchafuzi ule. Vivyo hivyo, ikiwa wewe utalinda afya ya kiroho ya watoto wako unahitaji kuwahami na ile “hewa” yenye sumu ya ulimwengu, ambayo inatapikwa mara nyingi sana kutoka kwenye televisheni.​—Mithali 13:20.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki