Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Yesu Anasali Akiwa na Huzuni Nyingi
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
    • Baada ya kufika kwenye sehemu hiyo maridadi yenye miti ya mizeituni, Yesu anawaacha nyuma mitume wanane. Labda wanabaki karibu na mwingilio wa bustani hiyo, kwa maana anawaambia hivi: “Ketini hapa, mimi naenda pale kusali.” Yesu anaenda na mitume watatu—Petro, Yakobo, na Yohana—anaingia ndani zaidi katika bustani. Anahuzunika sana na kuwaambia hivi wale mitume watatu: “Nimehuzunika sana, kiasi cha kufa. Kaeni hapa na mwendelee kukesha pamoja nami.”—Mathayo 26:36-38.

  • Yesu Anasali Akiwa na Huzuni Nyingi
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
    • Akiwa mbinguni, Yesu alijionea jinsi Waroma walivyowatesa sana watu na kuwaua. Sasa akiwa mwanadamu, aliye na hisia nyororo na anayeweza kuhisi uchungu, Yesu anaogopa jambo litakalompata. Hata hivyo, jambo muhimu zaidi ni kuwa anahuzunika kwa sababu anahisi kwamba akifa kama mhalifu anaweza kuliletea suto jina la Baba yake. Baada ya saa chache, atatundikwa kwenye mti kama mtu aliyemkufuru Mungu.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki