-
Kualikwa Kwenye Mlo—Mungu Anawaalika Nani?Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
-
-
“Mtu fulani alikuwa akiandaa mlo mkubwa wa jioni, naye akawaalika watu wengi. . . . Akamtuma mtumwa wake awaambie walioalikwa, ‘Njooni, kwa sababu kila kitu kiko tayari.’ Lakini wote wakaanza kutoa visingizio. Mmoja akasema, ‘Nilinunua shamba, ninahitaji kwenda kuliona; tafadhali, niwie radhi.’ Mwingine akasema, ‘Nimenunua jozi tano za ng’ombe, ninaenda kuwakagua; tafadhali, niwie radhi.’ Na bado mwingine akasema, ‘Nimetoka tu kuoa, kwa hiyo siwezi kuja.’”—Luka 14:16-20.
-
-
Kualikwa Kwenye Mlo—Mungu Anawaalika Nani?Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
-
-
Mfano ambao Yesu ametoa unaonyesha vizuri jinsi Yehova Mungu alivyomtuma Yesu Kristo kuwaalika watu ili wawe na tumaini la kuingia katika Ufalme wa mbinguni. Wayahudi, hasa viongozi wa kidini ndio waliokuwa wa kwanza kualikwa. Wengi wao walikataa mwaliko ambao Yesu alitoa katika kipindi chote cha huduma yake. Hata hivyo, watu wengine wangealikwa pia. Yesu anaonyesha wazi kwamba wakati ujao mwaliko wa pili utatolewa kwa watu wa hali ya chini wa taifa la Kiyahudi na wageuzwa imani pia. Baadaye, kutakuwa na mwaliko wa tatu na wa mwisho ambao utatolewa kwa watu ambao Wayahudi wanaona kuwa hawafai mbele za Mungu.—Matendo 10:28-48.
-