Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Apewa Mapokezi na Farisayo Mashuhuri
    Mnara wa Mlinzi—1988 | Desemba 15
    • Lo! ni udhuru bandia kama nini! Kwa kawaida shamba au mifugo huchunguzwa kabla haijanunuliwa, kwa hiyo hakuwi na uharaka wowote halisi wa kuitazama baadaye. Vivyo hivyo, ndoa ya mtu haipasi kumzuia asikubali mwaliko wa maana jinsi hiyo. Kwa hiyo anaposikia juu ya udhuru huo, bwana anakasirika na kumwamuru hivi mtumwa wake: “Toka nje uende barabarani na mipakani, ukawashurutishe kuingia ndani, nyumba yangu ipate kujaa. . . .

      Katika wale walioalikwa, hapana hata mmoja atakayeionja karamu yangu.”

  • Apewa Mapokezi na Farisayo Mashuhuri
    Mnara wa Mlinzi—1988 | Desemba 15
    • Zaidi ya watu wengine wote, wale waliokuwa wa kwanza kupokea mwaliko wa kuja katika mstari wa kupata Ufalme walikuwa viongozi wa kidini Wayahudi wa siku ya Yesu. Hata hivyo, wao walikataa mwaliko huo. Hivyo, kuanzia hasa Pentekoste 33 W.K., mwaliko wa pili ulitolewa kwa watu wenye kudharauliwa na walio dhalili wa taifa la Kiyahudi. Lakini walioitikia kujaza zile nafasi 144,000 katika Ufalme wa kimbingu wa Mungu hawakutosha. Kwa hiyo katika 36 W.K., miaka mitatu na nusu baadaye, mwaliko wa tatu ulio wa mwisho ulitolewa kwa watu wasiotahiriwa wasio Wayahudi, na kukusanywa kwao kukaendelea mpaka ndani ya karne ya 20. Luka 14:1-24.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki