-
“Yehova, Mungu Mwenye Rehema na Neema”Mnara wa Mlinzi—1998 | Oktoba 1
-
-
12, 13. Ni mambo gani ambayo yamesaidia watu fulani leo warudie fahamu zao? (Ona Sanduku.)
12 “Aliporudiwa na fahamu zake, alisema, ‘Ni wanaume wangapi walioajiriwa wa baba yangu ambao wanazidi katika kuwa na mkate, na huku mimi ninaangamia hapa kutokana na njaa kali! Hakika mimi nitainuka nifunge safari niende kwa baba yangu na kumwambia: “Baba nimefanya dhambi dhidi ya mbingu na dhidi yako wewe. Sistahili tena kuitwa mwana wako. Unifanye kama mmoja wa watu wako walioajiriwa.”’ Kwa hiyo akainuka akamwendea baba yake.”—Luka 15:17-20.
-
-
“Yehova, Mungu Mwenye Rehema na Neema”Mnara wa Mlinzi—1998 | Oktoba 1
-
-
14. Mwana mpotevu aliazimia kufanya nini, naye alionyeshaje unyenyekevu katika kufanya hivyo?
14 Lakini wale ambao wamepotea njia waweza kufanya nini kuhusu hali yao? Katika mfano wa Yesu wenye somo, mwana mpotevu aliamua kufunga safari ya kurudi nyumbani na kumwomba baba yake msamaha. “Unifanye kama mmoja wa watu wako walioajiriwa,” mwana mpotevu akaazimia kusema hivyo. Mtumishi aliyeajiriwa alikuwa kibarua, ambaye angeweza kufukuzwa baada ya kuarifiwa siku moja kimbele. Hiyo ilikuwa hali ya chini kuliko ya mtumwa ambaye, katika maana fulani, alikuwa kama mshiriki wa familia. Kwa hiyo, mwana mpotevu hakufikiria kuomba arudishwe kwenye hali yake ya zamani akiwa mwana. Angekuwa tayari kabisa kukubali hali ya chini zaidi, ili athibitishe upya uaminifu-mshikamanifu wake kwa baba yake siku kwa siku. Hata hivyo, mwana mpotevu alikuwa ashangae.
-