Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Wakati Mwana Mpotevu Anapopatwa
    Mnara wa Mlinzi—1989 | Februari 15
    • Kwa wakati huo, ‘mwana mkubwa wa baba alikuwako shambani.’ Ona kama unaweza kutambua yeye anawakilisha nani kwa kusikiliza sehemu iliyobaki ya hadithi. Yesu anasema hivi juu ya mwana huyo mkubwa: “Alipokuwa akija na kuikaribia nyumba, alisikia sauti ya nyimbo na machezo. Akaita mtumishi mmoja, akamwuliza, Mambo haya, maana yake nini? Akamwambia, Ndugu yako amekuja, na baba yako amemchinja ndama aliyenona, kwa sababu amempata tena, yu mzima. Akakasirika, akakataa kuingia ndani.

  • Wakati Mwana Mpotevu Anapopatwa
    Mnara wa Mlinzi—1989 | Februari 15
    • Lakini katika nyakati za ki-siku-hizi wana hao wawili wanawakilisha nani? Lazima iwe ni wale ambao wamepata kujua mambo ya kutosha juu ya makusudi ya Yehova hata wawe na msingi wa kuingia katika uhusiano pamoja naye. Mwana mkubwa anawakilisha washiriki fulani wa “kundi dogo,” au “kanisa [kundi, NW] la wazaliwa wa kwanza walioandikwa mbinguni.” Hao walichagua kufuata mwelekeo unaofanana na ule wa mwana mkubwa. Hawakutaka kukaribisha jamii ya kidunia, “kondoo wengine,” wakihisi kwamba hao walikuwa wakifanya wao waache kujulikana kwa umashuhuri mwingi kama zamani.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki