Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mwana Aliyepotea Arudi
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
    • Baba akizungumza na mwanawe mkubwa

      Wakati huo, mwana mkubwa wa yule baba yuko shambani. Yesu anasema hivi kumhusu: “Alipokuwa akirudi na kukaribia nyumba, akasikia sauti ya muziki na dansi. Basi akamwita mtumishi mmoja akamuuliza kilichokuwa kikiendelea. Akamjibu, ‘Ndugu yako amerudi, kwa hiyo baba yako amechinja ndama aliyenoneshwa kwa sababu amerudi akiwa na afya njema.’ Lakini akakasirika na kukataa kuingia ndani. Basi baba yake akatoka nje akaanza kumbembeleza. Akamjibu baba yake, ‘Tazama! nimekutumikia kwa miaka mingi na sijawahi kuvunja amri yako hata mara moja, lakini hujawahi kunipa hata mara moja mwanambuzi ili nijifurahishe pamoja na rafiki zangu. Lakini mara tu alipofika huyu mwanao aliyetumia vibaya mali yako na makahaba, ulimchinjia ndama aliyenoneshwa.’”—Luka 15:25-30.

      Ni nani ambao kama yule mwana mkubwa wamekuwa wakimshutumu Yesu kwa kuonyesha rehema na kushirikiana na watu wa kawaida na watenda dhambi? Ni waandishi na Mafarisayo. Yesu ametoa mfano huo kwa kuwa wanamshutumu kwa sababu ya kuwakaribisha watenda dhambi. Bila shaka, mtu yeyote anayemshutumu Mungu kwa kuonyesha rehema anapaswa kujifunza kutokana na mfano huo.

  • Mwana Aliyepotea Arudi
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
    • Yesu hasemi jambo ambalo mwishowe yule mwana mkubwa anafanya. Hata hivyo, baada ya Yesu kufa na kufufuliwa, “umati mkubwa wa makuhani wakawa waamini.” (Matendo 6:7) Huenda walitia ndani baadhi ya wale waliomsikia Yesu akisimulia mfano huo unaogusa moyo kuhusu mwana aliyepotea. Naam, iliwezekana kwao kurudiwa na fahamu, kutubu, na kumrudia Mungu.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki