-
Tajiri na LazaroMnara wa Mlinzi—1989 | Machi 15
-
-
Yesu anaeleza kwamba, “palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula sikuzote kwa anasa. Na maskini mmoja, jina lake Lazaro, huwekwa mlangoni pake, ana vidonda vingi, naye alikuwa akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri; hata mbwa wakaja wakamramba vidonda vyake.”
-
-
Tajiri na LazaroMnara wa Mlinzi—1989 | Machi 15
-
-
Jamii hii ya tajiri mwenye kiburi inawadharau kabisa kabisa maskini wenye cheo cha kawaida tu, wakiwaita ‛am ha·’aʹrets, au watu wa dunia. Hivyo Lazaro mwombaji maskini anawakilisha watu ambao viongozi wa kidini wanawanyima ulishaji wa kiroho unaofaa na mapendeleo. Kwa sababu hiyo, kama vile Lazaro aliyejawa na vidonda, watu wa cheo cha kawaida wanadharauliwa kuwa na maradhi ya kiroho na wenye kufaa kushirikiana na mbwa tu. Hata hivyo, wale wa jamii ya Lazaro wana njaa na kiu kwa ajili ya ulishaji wa kiroho na kwa hiyo wako langoni wakitafuta kupokea makombo yoyote haba ya chakula cha kiroho ambayo huenda yakaanguka kutoka meza ya tajiri.
-