Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mtoto Aliyeahidiwa
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
    • Zaidi ya mwezi mmoja unapita, na Yesu ana umri wa siku 40. Wazazi wake watampeleka wapi sasa? Watapanda naye kwenda katika hekalu huko Yerusalemu, ambalo liko kilomita chache kutoka mahali wanapoishi. Sheria inasema siku 40 baada ya mtoto mvulana kuzaliwa, mama yake alipaswa kutoa toleo la utakaso hekaluni.—Mambo ya Walawi 12:4-7.

      Maria anafanya hivyo. Anatoa ndege wawili wadogo, wakiwa toleo lake. Jambo hilo linaonyesha hali ya kiuchumi ya Yosefu na Maria. Kulingana na Sheria, walipaswa kutoa kondoo dume mchanga na ndege mmoja. Lakini ikiwa mama hangeweza kupata kondoo, angetoa njiwa-tetere wawili au hua wawili. Hivyo ndivyo anavyofanya Maria.

      “WAKATI ULIPOFIKA WA KUWATAKASA”

      Yosefu na Maria wanamleta mtoto Yesu hekaluni kwa ajili ya dhabihu ya utakaso

      Wanawake Waisraeli walipozaa, walionwa kuwa si safi kisherehe kwa kipindi fulani. Mwishoni mwa kipindi hicho, dhabihu ya kuteketezwa ingetolewa ikiwa dhabihu ya utakaso. Hivyo, wote walikumbushwa kwamba mtoto aliyezaliwa amerithi dhambi na kutokamilika. Mtoto Yesu alikuwa mkamilifu na mtakatifu. (Luka 1:35) Hata hivyo, Maria na Yosefu “wakamleta” hekaluni ili “kuwatakasa” kama walivyotakiwa na Sheria.—Luka 2:22.

  • Mtoto Aliyeahidiwa
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki