-
Alitimiza Tamaa ya Moyo WakeMnara wa Mlinzi—1994 | Machi 15
-
-
Mungu ameweka roho takatifu yake juu ya Simeoni na amemthawabisha kwa kumpa ufunuo. Simeoni hatakufa hadi atakapoona Yule atakayekuwa Mesiya. Lakini siku na miezi inapita. Simeoni anazeeka na hawezi kutazamia kuishi muda mrefu zaidi. Je! ahadi ya Mungu kwake itatimizwa?
-
-
Alitimiza Tamaa ya Moyo WakeMnara wa Mlinzi—1994 | Machi 15
-
-
Simeoni amchukua mtoto Yesu mikononi mwake kwa furaha kama nini! Huyu ndiye atakayekuwa Mesiya aliyeahidiwa—“Kristo wa Bwana [Yehova, NW].” Akiwa na umri mkubwa hivyo, Simeoni hawezi kutumaini kumwona Yesu akitimiza kusudi Lake la kidunia. Lakini, ni jambo zuri ajabu kumwona akiwa kitoto. Unabii mwingi wa Kimesiya unaanza kutimizwa. Simeoni ni mwenye furaha kama nini! Sasa ataridhika kulala katika kifo hadi ufufuo.—Luka 2:25-28.
-