Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mifano Miwili Kuhusu Mashamba ya Mizabibu
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
    • Baada ya kutoa mfano huo, Yesu anasimulia mfano mwingine. Pindi hii Yesu anaonyesha kwamba kosa la viongozi wa kidini sio tu kukataa kumtumikia Mungu. Kwa kweli wao ni waovu. Yesu anasimulia hivi: “Mtu fulani alipanda shamba la mizabibu akalizungushia ua, akachimba shinikizo la divai, akajenga mnara, kisha akalikodisha kwa wakulima, naye akasafiri kwenda ng’ambo. Majira yalipofika akatuma mtumwa kwa wakulima ili achukue kutoka kwao baadhi ya matunda ya shamba la mizabibu. Lakini wakamkamata, wakampiga na kumfukuza mikono mitupu. Akamtuma tena mtumwa mwingine kwao, na huyo wakampiga kichwani na kumwaibisha. Akamtuma mwingine, na huyo wakamuua, akawatuma wengine wengi, wakawapiga baadhi yao na kuwaua wengine.”—Marko 12:1-5.

      Je, wale wanaomsikiliza Yesu wataelewa mfano huo? Huenda wakakumbuka maneno haya ya shutuma yaliyosemwa na Isaya: “Shamba la mizabibu la Yehova wa majeshi ni nyumba ya Israeli; watu wa Yuda ndilo shamba alilolipenda sana. Aliendelea kutumaini haki itendwe, lakini tazama! kulikuwa na ukosefu wa haki.” (Isaya 5:7) Mfano wa Yesu unafanana na maneno hayo. Yehova ndiye anayemiliki shamba, nalo shamba la mizabibu ni taifa la Israeli, ambalo limezunguzishiwa ua na kulindwa na Sheria ya Mungu. Yehova aliwatuma manabii wawafundishe watu wake na kuwasaidia wazae matunda mazuri.

  • Mifano Miwili Kuhusu Mashamba ya Mizabibu
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
    • Hivyo, bila kujua wanajihukumu wao wenyewe, kwa maana wao ni kati ya “wakulima” wa “shamba la mizabibu” la Yehova, taifa la Israeli. Matunda ambayo Yehova anatazamia kutoka kwa wakulima hao yanatia ndani kumwamini Mwana wake, yaani, Masihi. Yesu anawatazama moja kwa moja viongozi hao wa kidini na kusema: “Je, hamkusoma kamwe andiko hili: ‘Jiwe ambalo wajenzi walilikataa, limekuwa jiwe kuu la pembeni. Hili limetoka kwa Yehova, na ni lenye kustaajabisha machoni petu’?” (Marko 12:10, 11) Kisha Yesu anakazia jambo kuu: “Ndiyo sababu ninawaambia, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu na kupewa taifa linalozaa matunda yake.”—Mathayo 21:43.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki