Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ufalme wa Mungu Utaanza Kutawala Dunia Lini?
    Mnara wa Mlinzi (Toleo la Watu wote)—2020 | Na. 2
    • Yesu alisema hivi: “Taifa litapigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme. Kutakuwa na matetemeko makubwa ya ardhi, na magonjwa na upungufu wa chakula katika sehemu mbalimbali.” (Luka 21:10, 11) Matukio hayo yote yangekuwa ishara isiyopingika kwamba “Ufalme wa Mungu umekaribia.” Je, matukio hayo yote yamewahi kutokea na kuonekana waziwazi ulimwenguni pote? Fikiria uthibitisho ufuatao.

  • Ufalme wa Mungu Utaanza Kutawala Dunia Lini?
    Mnara wa Mlinzi (Toleo la Watu wote)—2020 | Na. 2
    • 2. MATETEMEKO YA ARDHI

      Tetemeko la ardhi limesababisha nyumba ipate ufa.

      Makala ya Britannica Academic inasema kwamba, kila mwaka matetemeko makubwa ya ardhi yapatayo 100 hivi hutokea na kusababisha “uharibifu mkubwa.” Ripoti ya shirika moja la Marekani ilisema hivi; “Kulingana na rekodi zilizotunzwa kwa muda mrefu (tangu mwaka wa 1900), tunatarajia matetemeko makubwa ya ardhi 16 hivi kila mwaka.” Baadhi ya watu wanafikiri kwamba idadi ya matetemeko makubwa ya ardhi haijaongezeka lakini wanadamu wamebuni vifaa au njia bora za kugundua matetemeko hayo. Lakini ukweli ni kwamba matetemeko makubwa ya ardhi yanatokea ulimwenguni pote na yanasababisha vifo vya watu wengi sana na wengine wengi kuteseka.

      3. UPUNGUFU WA CHAKULA

      Chati inayoonyesha kushuka kwa uzalishaji wa mazao.

      Upungufu wa chakula hutokea ulimwenguni pote kwa sababu ya vita, ufisadi, kuporomoka kwa uchumi, kutozingatia kilimo bora, au kutokuwa na mipango inayofaa ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa. Ripoti ya Shirika la Chakula Duniani ya mwaka wa 2018 ilisema hivi kwa ufupi: “Watu milioni 821 duniani pote wanakabili janga la njaa na watu milioni 124 kati yao wameathiriwa zaidi.” Utapiamlo husababisha vifo vya watoto milioni 3.1 kila mwaka. Utapiamlo ulisababisha vifo vya asilimia 45 ya watoto waliokufa ulimwenguni pote katika mwaka wa 2011.

      4. MAGONJWA

      Alama za kibaolojia zinazoonyesha hatari na bakteria.

      Chapisho moja kutoka Shirika la Afya Duniani linaripoti hivi: “Tangu mwaka 2001 kumekuwa na magonjwa hatari ya mlipuko. Magonjwa yaliyosumbua zamani kama vile kipindupindu, ugonjwa wa tauni na homa ya manjano yamerudi, na magonjwa mengine mapya yameibuka, kama vile mafua ya ndege, mafua makali, MERS, Ebola na Zika.” Na hivi karibuni, janga la COVID-19. Ingawa wanasayansi na madaktari wana ujuzi mwingi kuhusiana na magonjwa, hawajaweza kupata tiba ya magonjwa yote.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki