Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi (Funzo)—2018 | Novemba
    • Mfadhili katika siku za Biblia

      Jioni ya mwisho kabla ya kifo chake, Yesu aliwashauri mitume wake wasijitafutie umashuhuri miongoni mwa waamini wenzao. Aliwaambia hivi: “Wafalme wa mataifa hupiga ubwana juu yao, na wale walio na mamlaka juu yao huitwa Wafadhili. Hata hivyo, ninyi hampaswi kuwa hivyo.”—Luka 22:25, 26.

  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi (Funzo)—2018 | Novemba
    • Hivyo basi, Yesu alimaanisha nini alipowaambia wanafunzi wake, “Ninyi hampaswi kuwa hivyo”? Je, Yesu alikuwa akimaanisha kwamba hawakupaswa kujishughulisha na masuala ya umma, yaani, hawakupaswa kuhangaikia hali za wanadamu wenzao kwa ujumla? Sivyo hata kidogo. Yesu alikuwa akirejezea nia iliyowafanya watu waonyeshe matendo hayo ya ukarimu.

      Katika siku za Yesu, matajiri walifadhili maonyesho na michezo iliyofanywa kwenye viwanja vikubwa, walijenga mabustani na mahekalu, na kutegemeza shughuli nyingine kama hizo wakiwa na nia ya kujijengea jina. Hata hivyo, lengo lao kuu lilikuwa kujijengea sifa, umashuhuri, na kupata kura. Kitabu kimoja cha marejeo kinasema, “Ingawa kulikuwa na mifano ya Wafadhili walioonyesha ukarimu wa kweli, kwa kawaida ukarimu wa aina hiyo ulichochewa na tamaa ya kutaka kujinufaisha kisiasa.” Roho kama hiyo ya kujitakia makuu na kujitanguliza ndiyo ambayo Yesu aliwahimiza wafuasi wake waepuke.

      Miaka kadhaa baadaye, mtume Paulo alikazia ukweli huo muhimu alipozungumza kuhusu kuwa na mtazamo unaofaa tunapotoa. Aliwaandikia hivi waamini wenzake huko Korintho: “Kila mmoja na afanye kama alivyoazimia moyoni mwake, si kwa kutopenda wala kwa kulazimishwa, kwa maana Mungu humpenda mtoaji mchangamfu.”—2 Kor. 9:7.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki