Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Yesu Anasali Akiwa na Huzuni Nyingi
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
    • Yesu anahangaishwa sana na jinsi kifo chake kama mhalifu kitakavyoliletea suto jina la Baba yake. Ingawa hivyo, Yehova anasikiliza sala ya Mwana wake, na pindi moja Mungu anamtuma malaika ili amtie nguvu. Hata hivyo, Yesu haachi kumsihi Baba yake, bali anaendelea “kusali kwa bidii zaidi.” Ana mkazo mwingi sana wa kihisia. Yesu amebeba jukumu zito sana! Uhai wake mwenyewe wa milele na uhai wa wanadamu wenye imani unahusika. Hata ‘jasho lake linakuwa kama matone ya damu yakidondoka chini.’—Luka 22:44.

  • Yesu Anasali Akiwa na Huzuni Nyingi
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
    • JASHO KAMA MATONE YA DAMU

      Daktari Luka haelezi jinsi jasho la Yesu lilivyokuwa “kama matone ya damu.” (Luka 22:44) Huenda Luka alikuwa akizungumza kwa njia ya mfano, kwamba jasho hilo lilikuwa kama damu inayodondoka kutoka kwenye kidonda. Wazo lingine lilitolewa na Dkt. William D. Edwards katika kitabu The Journal of the American Medical Association (JAMA): “Ingawa hili ni tukio lisilo la kawaida, jasho lenye damu (hematidrosisi . . . ) linaweza kutoka mtu anapokuwa na hisia nyingi . . . Damu inapovuja na kuingia katika mishipa ya jasho, ngozi inakuwa laini na kupasuka kwa urahisi.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki