-
“New World Translation” ya Utaalamu na Yenye Kufuatia HakiMnara wa Mlinzi—1991 | Machi 1
-
-
Katika Luka 4:18, kulingana na New World Translation, Yesu alitumia kwake mwenyewe unabii katika Isaya, akisema hivi: “Roho ya Bwana MUNGU [Yehova, NW] i juu yangu.” (Isaya 61:1) Wengi hupinga utumizi wa jina la Yehova hapa. Hata hivyo, hapo ni pamoja pa mahali 200 ambapo jina hilo hutokea katika New World Translation ya Maandiko ya Kigiriki ya Kikristo, yanayoitwa eti Agano Jipya. Ni kweli kwamba, hakuna hati-mkono ya mapema ya Kigiriki iliyopo bado ikiwa na jina la kibinafsi la Mungu. Lakini jina hilo lilitiwa ndani katika New World Translation kwa sababu zilizo imara, si kwa ajili ya mawazo ya kigeni tu. Na wengine wamefuata mwendo uo huo. Katika lugha ya Kijerumani tu, angalau tafsiri 11 zinatumia “Yehova” (au utohozi wa herufi za Kiebrania, “Yahweh”) katika maandishi ya “Agano Jipya,” hali watafsiri wanne wanaongeza jina hilo katika mabano baada ya “Bwana.”c Watafsiri Wajerumani zaidi ya 70 hulitumia katika vielezi-chini au katika mafafanusi.
-
-
“New World Translation” ya Utaalamu na Yenye Kufuatia HakiMnara wa Mlinzi—1991 | Machi 1
-
-
c Johann Babor, Karl F. Bahrdt, Petrus Dausch, Wilhelm M. L. De Wette, Georg F. Greisinger, Heinrich A. W. Meyer, Friedrich Muenter, Sebastian Mutschelle, Johann C. F. Schulz, Johann J. Stolz, na Dominikus von Brentano. August Dächsel, Friedrich Hauck, Johann P. Lange, na Ludwig Reinhardt wana jina hilo katika mabano.
-