Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Je, Wajua?
    Mnara wa Mlinzi—2010 | Machi 1
    • Kwa nini Yesu alisema kwamba “hakuna anayeweka divai mpya ndani ya viriba vya divai vilivyozeeka”?

      ▪ Katika nyakati za Biblia, kwa kawaida divai ilihifadhiwa ndani ya ngozi ya wanyama. (Yoshua 9:13) Chupa za ngozi zilitengenezwa kwa ngozi za wanyama wa kufugwa kama vile mwana-mbuzi au mbuzi. Ili kutengeneza chupa ya ngozi, kichwa na miguu ya mnyama aliyekufa ilikatwa kisha ngozi ilitolewa kwa uangalifu bila kutoboa tumbo. Ngozi hiyo ilitengenezwa vizuri na mashimo yote yalishonwa isipokuwa sehemu ya shingo au ya mguu wa mnyama. Sehemu hiyo haikushonwa ili iwe mdomo wa chupa hiyo. Shimo hilo lingeweza kufungwa kwa kifuniko au kamba.

      Baada ya muda, ngozi hiyo ilikauka na kuwa ngumu. Kwa hiyo, chupa za ngozi au viriba vilivyozeeka havikufaa kuwekwa divai mpya, ambayo inaendelea kuchacha. Divai iliyokuwa ikichacha ingepasua ngozi iliyokauka ya viriba vilivyozeeka. Lakini, viriba vipya vilikuwa laini zaidi na vingeweza kustahimili nguvu za divai mpya iliyokuwa ikichacha. Kwa hiyo, Yesu alisema jambo ambalo watu wote walijua katika siku zake. Alisema jambo linalotukia wakati mtu anapoweka divai mpya katika viriba vilivyozeeka: “Ndipo divai mpya itavipasua viriba vya divai, nayo itamwagika navyo viriba vya divai vitaharibika. Lakini divai mpya lazima iwekwe ndani ya viriba vipya vya divai.”—Luka 5:37, 38.

  • Je, Wajua?
    Mnara wa Mlinzi—2010 | Machi 1
    • [Picha katika ukurasa wa 15]

      Kiriba kilichozeeka

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki