Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Yesu Ajapo Katika Utukufu wa Ufalme
    Mnara wa Mlinzi—1997 | Mei 15
    • 4 Wale mitume watatu waliona nini hasa? Ufuatao ni ufafanuzi wa Luka wa hilo tukio: “[Yesu] alipokuwa akisali kuonekana kwa uso wake kukawa tofauti na vao lake likawa jeupe kwa kumeremeta. Pia, tazama! wanaume wawili walikuwa wakiongea naye, waliokuwa ni Musa na Eliya. Hawa walionekana wakiwa na utukufu nao wakaanza kuongea juu ya kuondoka kwake alikokusudiwa kutimiza Yerusalemu.” Kisha “wingu lilifanyika na kuanza kuwafunika kivuli [hao mitume]. Walipokuwa wakiingia katika wingu, wakawa wenye hofu. Na sauti ikaja kutoka katika lile wingu, ikisema: ‘Huyu ni Mwana wangu, yule ambaye amechaguliwa. Msikilizeni yeye.’”—Luka 9:29-31, 34, 35.

  • Yesu Ajapo Katika Utukufu wa Ufalme
    Mnara wa Mlinzi—1997 | Mei 15
    • 5. Mgeuko-umbo ulimwathirije mtume Petro?

      5 Mtume Petro tayari alikuwa amemtambua Yesu kuwa “Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.” (Mathayo 16:16) Maneno ya Yehova kutoka mbinguni yalithibitisha utambulisho huo, na ono la kugeuka umbo kwa Yesu lilikuwa mwonjo wa kimbele wa kuja kwa Kristo katika nguvu na utukufu wa Ufalme, kuwahukumu wanadamu hatimaye. Miaka zaidi ya 30 baada ya mgeuko-umbo, Petro aliandika hivi: “Haikuwa kwa kufuata hadithi zisizo za kweli zilizotungwa kwa usanifu mwingi kwamba tuliwafahamisha nyinyi juu ya nguvu na kuwapo kwa Bwana wetu Yesu Kristo, lakini ilikuwa kwa kupata kuwa mashahidi wa kujionea fahari yake. Kwa maana alipokea kutoka kwa Mungu Baba heshima na utukufu, wakati maneno ya namna hii yalipopelekwa kwake kwa utukufu wenye fahari: ‘Huyu ni mwana wangu, mpendwa wangu, ambaye mimi mwenyewe nimemkubali.’ Ndiyo, maneno haya tuliyasikia yakipelekwa kutoka mbinguni tulipokuwa tungali pamoja naye katika mlima mtakatifu.”—2 Petro 1:16-18; 1 Petro 4:17.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki