Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Yesu Alizaliwa Wapi na Wakati Gani?
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
    • Kaisari Augusto, maliki wa Milki ya Roma, ameagiza kwamba kila mtu anapaswa kuandikishwa. Basi Yosefu na Maria wanapaswa kusafiri hadi jiji alikozaliwa Yosefu, jiji la Bethlehemu, upande wa kusini wa Yerusalemu.

      Watu wengi wamekuja Bethlehemu ili kuandikishwa. Sehemu pekee ya kukaa ambayo Yosefu na Maria wanapata ni katika zizi, ambako punda na wanyama wengine huwekwa. Yesu anazaliwa hapo. Maria anamfunga kwa vitambaa na kumlaza katika hori, mahali ambapo chakula cha wanyama huwekwa.

      Lazima iwe kwamba Mungu alihakikisha Kaisari Augusto anaagiza watu waandikishwe. Kwa nini? Kwa sababu hilo lilifanya iwezekane kwa Yesu kuzaliwa huko Bethlehemu, jiji alikozaliwa Mfalme Daudi, babu yake. Maandiko yalikuwa yametabiri zamani kwamba Mtawala aliyeahidiwa angezaliwa katika jiji hilo.—Mika 5:2.

  • Yesu Alizaliwa Wapi na Wakati Gani?
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
    • Watu wengi leo wanaamini kwamba Yesu alizaliwa Desemba 25. Lakini katika eneo la Bethlehemu, Desemba ni kipindi cha mvua na baridi. Pindi nyingine, hata kunakuwa na theluji. Wakati kama huo wa mwaka, wachungaji hawangekuwa nje malishoni usiku pamoja na wanyama wao. Pia, haiwezekani kwamba maliki Mroma angewaagiza watu ambao tayari walikuwa na mwelekeo wa kumwasi wasafiri kwa siku nyingi katika majira ya baridi kali ili waandikishwe. Inaonekana kwamba Yesu alizaliwa Oktoba.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki