Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Msamaria Athibitika Kuwa Jirani Mwema
    Mnara wa Mlinzi—1998 | Julai 1
    • Kwa sababu ya hali hiyo, maneno ya Yesu kwa mtu mwenye ujuzi mwingi katika sheria ya Kiyahudi ni yenye kuelimisha sana. Huyo mwanamume alimfikia Yesu na kumwuliza hivi: “Mwalimu, ni kwa kufanya nini mimi nitarithi uhai udumuo milele?” Kwa kujibu, Yesu alimwelekeza kwenye Sheria ya Kimusa, ambayo hutoa agizo la ‘kumpenda Yehova kwa moyo wako wote, nafsi, nguvu, na akili,’ na ‘kupenda jirani yako kama wewe mwenyewe.’ Ndipo huyo mwanasheria akamwuliza Yesu: “Ni nani kwa kweli aliye jirani yangu?” (Luka 10:25-29; Mambo ya Walawi 19:18; Kumbukumbu la Torati 6:5) Kulingana na Mafarisayo, neno “jirani” lilitumiwa kuwahusu wale tu walioshika mapokeo ya Kiyahudi—kwa hakika si kuwahusu wasio Wayahudi au Wasamaria. Kama mwanasheria huyo mwenye udadisi alifikiri kwamba Yesu angeunga mkono maoni yake, jambo la kushangaza lilimngoja.

  • Msamaria Athibitika Kuwa Jirani Mwema
    Mnara wa Mlinzi—1998 | Julai 1
    • Somo Kwetu

      Mwanamume aliyemwuliza Yesu maswali alifanya hivyo katika jitahada ya kutaka “kujithibitisha mwenyewe kuwa mwadilifu.” (Luka 10:29) Labda alifikiri kwamba Yesu angesifu kufuata kwake kwa uangalifu sana Sheria ya Kimusa. Lakini mtu huyu mwenye kujitanguliza alihitaji kujua ukweli wa mithali hii ya Biblia: “Kila njia ya mtu ni sawa machoni pake mwenyewe; bali BWANA huipima mioyo.”—Mithali 21:2.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki