Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Msamaria Athibitika Kuwa Jirani Mwema
    Mnara wa Mlinzi—1998 | Julai 1
    • Yesu aliendelea kusema hivi: “Msamaria fulani mwenye kusafiri katika ile barabara alikuja akamkuta.” Bila shaka kutajwa kwa Msamaria kuliongeza udadisi wa huyo mwanasheria. Je, Yesu angekubali maoni yasiyofaa ya jamii hiyo? Kinyume cha hilo, huyo Msamaria alipomwona msafiri aliyepatwa na msiba “akasukumwa na sikitiko.” Yesu akasema hivi: “Kwa hiyo akamkaribia akafunga majeraha yake, akimwaga mafuta na divai juu yayo. Kisha akampandisha juu ya hayawani wake mwenyewe akamleta kwenye hoteli ndogo na kumtunza.b Na siku iliyofuata akatoa dinari mbili, akampa hizo mtunza-hoteli, na kusema, ‘Mtunze, na chochote kile utumiacho mbali na hiki, mimi nitakulipa nirudipo hapa.’”—Luka 10:33-35.

  • Msamaria Athibitika Kuwa Jirani Mwema
    Mnara wa Mlinzi—1998 | Julai 1
    • b Ni wazi kwamba hoteli fulani katika siku ya Yesu ziliandaa si mahali pa kujisetiri tu, bali pia chakula na huduma nyingine. Hiyo yaweza kuwa aina ya makao ambayo Yesu alikuwa akifikiria, kwa maana neno la Kigiriki lililotumiwa hapa ni tofauti na lile litafsiriwalo “chumba cha makao” kwenye Luka 2:7.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki